Saturday, October 18, 2014

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO LAKANUSHA UVUMI WA UJUMBE MFUPI WA MANENO

Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania limekanusha uvumi wa ujumbe mfupi wa maneno unaoendelea kusambazwa kwenye simu na mitandao ya kijamii kuhusiana na Papa kumtaka Rais Barack Obama wa Marekani kupitisha sheria ya kuabudu siku ya jumapili mwezi huu.

Akizungumza katika kipindi cha Kanisani jumahili kupitia Morning Star Radio ambacho huwapatia nafasi Viongozi mbalimbali wa Kanisa hilo kutoa mada na kuulizwa maswali na wasikilizaji Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji James Machage amesema kuwa ujumbe huo ni uvumi na wa uongo ambao hauhusiana na kanisa hilo,kwani kanisa lina utaratibu maalum wa kutoa matamko yanayolihusu na sio katika ujumbe wa maneno katika simu ama kwenye mitandao ya kijamii.

Toka jumatano iliyopita blog hii imekuwa ikitumiwa na kushuhudia ujumbe huo ambao mwanzoni ulikuwa kwa lugha ya kiingereza na ijumaa ukawa umetafsiriwa kwa lugha ya kiswahili hali ambayo imeleta sintofahamu miongoni mwa waumini wa kanisa la Waadventista Wa Sabato

Ujumbe wenyewe wa kiingereza "Doreen Emmau: The Pope urging US President Barrack Obama to pass the National Sunday Law this month,SDA President Ted Wilson is appealing to all SDA members around the world to pray and have a personal consecration and revival and reformation of Godliness for 7 days either 7 am or 7 pm for the outcome of the Holy Spirit in the form of the latter rain.Plse send to all SDA members.Many will be cold in faith,a prophecy that will go back to the fold of the Beast the pope itself.Be Watchful my friend,Jesus is at the Door....He is coming be Ready....Harry Coombs" 

Wa kiswahili  "Papa amwomba rais wa marekani Barack Obama atangaze sheria ya taifa ya jumapil mwisho wa mwezi huu, rais wa wasabato Ted wilson anawaomba waadventista wasabato duniani kote kufanya maombi na matengenezo kwa siku saba kwa ajili ya utauwa wa kweli muda wa maombi ni saa 1 asbh au 1 jioni kwa kumwagwa roho mtakatifu kwa namna ya mvua.Tafadhali tuma sms kwa waadventista wasabato.Rafiki yangu kesha na uwe tayari YESU anakuja yuko mlangoni"

Naye Katibu Mkuu wa Konferensi ya Mashariki mwa Tanzania Mchungaji Sadock Butoke amesema jana kuwa kanisa hilo halina taarifa hizo na ujumbe huo unapaswa kupuuzwa. 
  

Popular Posts

Labels