(Picha na:Facebook) |
Internet.org iliyozinduliwa Oktober 29 mwaka huu ni mpango wa kimataifa unaoyashirikisha miongoni mwa makampuni makubwa ya teknolojia, taasisi zisizo za kibiashara zinazofanya kazi pamoja kufikisha huduma ya internet kwa mabilioni ya watu duniani ambao hawapati huduma ya internet.
Kampuni ya mtandao wa kijamii ya Facebook yenye makao yake nchini Marekani ni waanzilishi wa program tumishi ya internet.org ambayo ilianza kutumika barani Afrika katika nchi ya Zambia julai mwaka huu kwa wateja wa mtandao wa Airtel inawezesha mtumiaji wa simu za viganjani kupata taarifa za Afya,Elimu,Uchumi,ajira,mawasiliano bila ya kutozwa gharama za kimtandao.
Taarifa ya hivi karibuni kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania - TCRA, ilionyesha kuwa idadi ya watu wanaotumia internet iliongezeka kutoka milioni saba na nusu mwaka 2012 mpaka kufikia milioni tisa nukta tatu mwaka huu 2014.
Taarifa ya Facebook imeeleza kuwa huduma zinazokuwa zikipatikana bure kwa wateja wa Tigo ni katika program tumishi ya Internet.org ni
- AccuWeather
- BabyCenter & MAMA
- BBC News & BBC Swahili
- BrighterMonday
- The Citizen
- Facts for Life
- Girl Effect
- Messenger
- Mwananchi
- Mwanaspoti
- OLX
- Shule Direct
- SuperSport
- Tanzania Today
- Wikipedia