Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Tekinolojia nchini Tanzania imeahidi kutoa msaada kwa shirika la posta nchini humo ili liweze kuwa shirika bora na la kisasa zaidi.
Akizungumza katika
warsha maalumu ya kuadhimisha siku ya posta duniani iliyofanyika jijini Dar es salaam Katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano sayansi
ya tekinolojia Profesa Partick Makungu amesema kuwa wizara yake ipo tayari
kuliboresha shirika hilo ambalo ndilo
lililo na uwezo mkubwa wa kumfikia kila mwananchi katika
sehemu tofauti.
Profesa
Makungu amewataka viongozi wa shirika hilo pamoja na wadau wengine kutambua
kuwa idadi kubwa ya watanzania wanaishi katika maeneo ya vijijini, hivyo wanawajibu wa kuhakikisha wanaboresha miundo mbinu ambayo itasaidia kuwezesha
shughuli za utumaji wa vifurushi kuwa wa rahisi na wa haraka zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo
Deusi Mndeme amesema lengo lao kubwa
kama viongozi wa shirika ni kuliboresha ili liwe la kisasa liweze
kuhudumia idadi kubwa zaidi ya watanzania
kwani pamoja na uwepo wa tekinolojia mpya za mawasiliano bado lipo hitaji kubwa
kwa wananchi kutuma vifurushi kwa njia
ya posta,
Siku ya posta duniani huadhimishwa kila tarehe
9 Oktoba kila mwaka ambapo mwaka huu siku hiyo imeadhimishwa hii leo Jijini DSM
ikiwa na kauli mbiu isemayo “ posta katika
mageuzi ya sekta ya mawasiliano”.