Oktoba 11,2014 ilikuwa ni siku maalum kwa waumini wa
Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani kwa ajili ya kuombea
waathirika wa ugonjwa wa ebola,tukio hilo liliwashirikisha watu wote duniani kwa kushiriki kwa kutumia mitandao ya kijamii wa twitter na facebook kwa kutumia #UnitedinPrayer for #EbolaCrisis
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani
Mchungaji Ted Wilson hivi karibuni ambaye anaongoza kanisa hilo lenye waumini
milioni 18 katika nchi 215 kutoka divisheni 13 za kanisa hilo duniani amesema
ameguswa sana na tatizo la Ebola lililowakumba watu kutoka nchi za Afrika
magharibi hasa nchi za Guinea,Siera Leone, Liberia ,Senegal na Nigeria.
Octoba
mosi mwaka huu kanisa la waadventista wa sabato kupitia chama cha wachungaji lilianzisha mkakati wa
kufanya maombi duniani kote kwa kutumia mitandao ya kijamii kuombea tatizo la
ugonjwa wa ebola kwa watu waliokumbwa na
ugonjwa huo,mkakati ambao umehitimishwa oktoba
11,2014 kwenye makao makuu ya kanisa hilo na viongozi wa ngazi za juu toka
sehemu mbalimbali duniani waliokutana yalipo makao makuu ya kanisa hilo
Maryland nchini Marekani