Kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika,Raia wa Afrika kutoka Congo-DRC Verone Mankou,amezindua simu aina ya smarthphone na kompyuta za tablet.
Kampuni yake ya VMK inatumia vifaa vinavyoendeshwa kwa teknolojia ya Adroad ya Kampuni ya Google
Simu hizo za smartophone zitauzwa kwa bei ya rejareja ya dola za kimarekani 170 sawa na shilingi 268,600 hivi za Tanzania.
Mankou aliyekuwa katika mkutano wa Tech4Afrika uliofanyika mjini Johannesburg hivi karibuni anasema ni waafrika wenyewe ndio watakaofahamu mahitaji ya afrika .
"Apple ni kampuni kubwa Marekani,Samsung ni barani Asia na tunataka VMK kuwa kampuni kubwa barani Afrika"anasema mvumbuzi huyo.
Simu hiyo ya smartphone nyumba na mbele ina kamera na skrini ya ukubwa wa inchi 3.5 sawa na sentimita 8.9,kuna mipango ya kuuza simu hizi katika nchi kumi za Afrika Magharibi pamoja na Ubelgiji,Ufaransa na India.
Mankou anasema anatajia kuzindua uuzaji wa kompyuta za bei nafuu zaidi kwa wanafunzi mapema mwaka huu.
VMK imesisitiza kuwa wakati bidhaa zake zinatengenezwa China kwa sababu za unafuu wa gharama ubunifu na uhandisi wa simu hizo ni wa kiafrika.