Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa viwango vipya vya bei
elekezi ya gharama za kupiga simu kwa mwingiliano wa mitandao ya
mawasiliano katika kampuni mbalimbali za simu nchini. Bei hizo
zitakazoanza kutumika kuanzia Machi mosi mwaka huu, zitadumu hadi
Desemba 31, mwaka 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, aliwaambia waandishi wa habari jana, kwamba lengo na uwepo wa gharama hizo ni kuwapunguzia gharama watumiaji wa mitandao ya simu.
Kwa mujibu wa Profesa Nkoma, viwango hivyo vitasaidia kupunguza gharama za kupiga simu kwa mitandao yote ya simu bila kujali ukubwa wa kampuni.
Chini ya gharama hizo mpya, alisema kuanzia Machi Mosi, gharama za kupiga simu kwa dakika moja kutoka kampuni moja ya simu kwenda mtandao wowote itagharimu Sh 34.92.badala ya Sh 112 kwa dakika.
“Kuanzia Januari mosi mwaka 2014, zitakuwa ni shilingi 32.40, Januari mosi mwaka 2015, itakuwa ni shilingi 30.58, Januari mosi mwaka 2016, itakuwa ni shilingi 28.57 na hadi kufikia Januari mosi mwaka 2017, gharama ya kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine itakuwa shilingi 26.96 kwa dakika badala ya Sh 112 ya sasa.
Profesa Nkoma alisema kwamba, kutokana na kupanuka kwa sekta ya mawasiliano nchini, kumesababisha liwepo ongezeko la watumiaji wa simu na kwamba hatua hiyo imeifanya TCRA kuangalia jinsi ya kuwasaidia watumiaji wa simu.
"Ingawa siyo kazi yetu kupanga viwango vya gharama za kupiga simu, inapofika hatua fulani ni lazima tuwajibike kwa kuwa sisi ni kama mdhibiti mkuu wa mawasiliano nchini, ingawa pia jambo hili linapaswa kushughulikiwa na wenye kampuni husika.
"Kwa kuwa wenye kampuni za simu walishindwa kukubaliana ndani ya muda tuliowapangia, tumeamua kupanga viwango hivi sisi wenyewe, kwani tumeona jinsi wananchi wanavyopata shida katika kuwasiliana pindi mmoja wapo anapokuwa mtandao wa simu tofauti na wa mwenzake.
“Tumelazimika kufanya hivi kwa sababu mtu anapokuwa katika mtandao fulani na kumpigia aliye mtandao mwingine, anakatwa kiwango kikubwa cha fedha, hii siyo sawa.
“Tunaamini viwango hivi nafuu vya gharama za kupiga simu kwa mitandao tofauti vitawasaidia watumiaji wengi wa simu, kwani wengi wao wamejikuta wakiingia gharama zisizo na ulazima kutokana na kuwepo kwa makato makubwa ya gharama za kupiga simu pindi wanapofanya mawasiliano ya kuingiliana na kampuni tofauti za simu.
"Unakuta mtu mmoja ana zaidi ya simu mbili na anafanya hivyo kwa lengo la kuepuka gharama za makato kutoka kwenye mitandao hiyo, kwani unakuta gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja hadi mwingine ni kubwa ukilinganisha na gharama za kupiga mtandao huo huo.
"Kwa hiyo, punguzo hili litamsaidia mtumiaji wa simu awe na uhuru wa kutumia simu moja au laini ya mtandao mmoja kwa ajili ya mawasiliano na mtu wa mtandao mwingine kwa gharama hizi kulingana na dakika atakayoongea.
“Wananchi wajue kwamba, hii ni mara ya tatu tangu tuanze kutoa viwango vipya vya mabadiliko ya gharama za kupiga simu kwa mwingiliano wa mawasiliano katika kampuni za simu hapa nchini.
"Kwa mara ya kwanza kufanya mabadiliko haya ilikuwa mwaka 2004, mara ya pili ilikuwa 2008 na mara ya tatu imekuwa ni mwaka huu,” alisema.
Pamoja na TCRA kupanga viwango hivyo, alisema kampuni za simu za mkononi zinatakiwa kuchukulia uamuzi huu kama changamoto katika soko la ushindani wa biashara kwa kuwa zina ushindani wa kibiashara.
"Kampuni za simu zinatakiwa kuboresha huduma na kubuni njia mbadala za kuweza kukabiliana na ushindani wa soko kwa kipindi hiki, kwa kuwa bado tumetoa fursa kwa kampuni hizo kuwasilisha makubaliano yao kwetu juu ya viwango hivyo vipya tulivyovitoa na mwisho wa kufanya hivyo ni Machi 31, mwaka 2013.

Hatua hiyo ya TCRA, imekuja baada ya kampuni za simu za mikononi
kushindwa kukubaliana namna ya kurejesha makubaliano waliyoyafikia juu
ya upangaji wa viwango vipya vya bei za kupiga simu kutoka mtandao mmoja
kwenda mtandao mwingine.
Chini ya makubaliano hayo, kampuni za simu zilitakiwa kurudisha majibu kabla ya kuanza kwa mwaka 2013 viwango halisi vya gharama hizo vipatikane.