Nchi ya Kenya imechukua hatua ya kwanza katika ujenzi wa kile kinachotarajiwa utakuwa mradi mkubwa zaidi barani Afrika wa mji wa kiteknolojia (Silicon Valley) au unaotegemea sana vifaa vya electroniki katika kuendeleza teknolojia ya habari na mawasiliano.
Rais Mwai Kibaki alizindua rasmi mradi huo katika eneo la Konza,mtaa mdogo kusini mwa Nairobi,ambako mji huo mpya wa kiteknolojia utajengwa katika muda wa miaka 20 ijayo.Rais Kibaki ambaye alizindua mradi huo muda mfupi kabla ya kuondoka madarakani mwezi machi alieleza mji wa Konza utasaidia kubadili uchumi wa Kenya kwa kiasi kikubwa.
Mradi huu wenye thamani ya Dola bilioni kumi na nne na nusu upo chini ya mpango wa Wizara ya Habari na Mawasiliano.Mradi huo unasemekana kutoa nafasi zaidi ya 100,000 za ajira ifikapo mwaka 2030 pamoja na kuendelea kudumisha ukuaji wa pato la nchi la jumla ya aslimia 10 katika kipindi cha miaka 18 ijayo.