Mkurugenzi wa Mawasiliano TCRA, Innocent Mungy |
Mkurugenzi wa Mawasiliano TCRA, Innocent Mungy, alisema hayo wakati wa mahojiano yake na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa wananchi wanapaswa kujiandaa mapema ili kuepusha usumbufu kama ulio jitokeza kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
“Tumeshuhudia usumbufu mkubwa ulio jitokeza hapa Dar, watu wengi walikuwa bado hawana uelewa wa jinsi ya kuvitumia ving’amuzi na wengine mpaka siku ya kuzima mitambo inafika bado hawajanunua,” alisema na kuongeza: “Wengine tulikwenda kuwatembelea na kukuta hata umeme hajawasha ukutani, mwingine hajui kuchomeka zile nyaya, Kwa kweli ni changamoto kubwa.”
Mungy alisema licha ya changamoto ya uelewa mdogo wa watu, kwa sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani yamebaki maeneo machache yenye matatizo madogo madogo na baada ya kukamilisha itafuatia mikoa ya Tanga na Dodoma.
“Bahati mbaya jiji la Dar limekuwa la kwanza katika zoezi hili, lakini tunaenda hatua kwa hatua baada ya kukamaliza hapa tutahamia Tanga na Dodoma hivyo wananchi wa mikoa hiyo watakuwa wamejifunza kutoka kwa wenzao wa Dar es Salaam,” alisema.
“Masuala ya malipo ya kila mwezi ya king’amuzi siyo ya lazima, kitu cha lazima ni malipo ya kusaidia kuiruhusu kadi ya mteja kufanya kazi, endapo atahitaji kuona chanali za ziada, atalazimika kulipia ili aweze kuzipata,” alisema Mungy.
Chanzo:
NIPASHE