Mitandao ya whatsapp na viber huenda
ikadhibitiwa Afrika Kusini ikitegemea matokeo ya vikao vya bunge
baadaye mwezi huu, umeripoti mtandao unaoheshimika wa Fin24.
Kampuni mbili kubwa za simu Afrika kusini Vodacom na MTN mwaka uliopita zilitoa wito wa kudhibitiwa kwa huduma hizo.
Kuna hawa washiriki wanaopata manufaa makubwa katika sekta hii bila kutumia pesa. Tutapataje usawa?" afisa mmoja wa MTN alinukuliwa akisema.Kamati ya bunge kuhusu mawasiliano ya posta ilipanga kufanya kikao hicho tarehe 26 mwezi January kujadili sera za kuingilia kati swala hilo.
Chanzo:BBC