Tuesday, January 5, 2016

ELIMU DUNI YA MTANDAO CHANZO CHA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII



 

Wadau mbalimbali wa mitandao ya kijamii jijini Arusha wameeleza kuwa, Elimu duni kuhusu matumizi ya mtandao ndio chanzo cha matumizi mabaya ya mitandao hiyo hali inayosababisha migogoro katika jamii. 

Akizungumzia suala hilo Bwana Fransis Kimati ameeleza kuwa elimu duni kuhusu mitandao ikiwemo ukuaji wa sayansi na Teknolojia ndio chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili hususani kwa vijana. 

Kwa upande wake Bw. Joshua Jacob ambaye ni mwandishi wa vitabu amesema, hatua zinataikiwa kuchukuliwa ikiwemo utolewaji elimu kwa rika la vijana ambao ndio kundi kubwa la watumiji wa mitandao, kupitia vitabu, majarida warsha na matamasha mbalimbali, ili kubadilisha mitazamo mibaya kwa vijana.

Aidha wamesema kuwa dhamira ya kuwepo mitandao ya kijamii mbalimbali ikiwemo Facebook,Twiter ni nzuri lakini bado jamii haijawa na ufahamu wa kutumia mitandao hiyo kwa kujiendeleza katika njanja mbalimbali.

Popular Posts

Labels