Thursday, January 14, 2016

TTCL YAKOPA DOLA MILIONI 22 KUSAMBZA MTANDAO WA 3G NA 4G LTE

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/01/bt.jpg
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB), Jaffer Machano mara baada ya kutiliana saini.

Kampuni ya Simu Tanzania TTCL na Benki ya TIB zimetiliana saini Mkataba wa makubaliano ya dhamana ya Benki na Mkopo wa Dola za Marekani Milioni 22 ikiwa ni awamu ya kwanza ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 329 itakazopewa TTCL.

Akizungumza katika hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya mkopo huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema mkopo huo ni mahususi kwa ajili ya kuiwezesha TTCL kusimika mitambo mipya na ya kisasa kuboresha huduma zake kwa kujenga na kusambaza huduma za  Mitandao ya 3G na 4G LTE  nchini kote.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Jaffer Machano amesema katika kutimiza wajibu wa TIB kama benki ya maendeleo, ujenzi wa miundombinu umepewa kipaumbele na hii ni pamoja na miundombinu ya sekta ya Mawasiliano.

Baadhi ya huduma za TTCL zitakazoimarika baada ya uwezeshaji huu ni pamoja huduma za simu na intaneti yenye kasi kubwa inayowezesha huduma za kijamii kufanyika kwa urahisi kwa njia ya mtandao.

 Huduma kama vile za Elimu kwa njia ya mtandao (E education), Afya kwa njia ya mtandao (E health) na huduma katika Sekta nyingine za kiuchumi kama vile Biashara, Viwanda na Kilimo nazo zitanufaika sana ambapo wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali watapata Mawasiliano ya uhakika katika kufanikisha shughuli zao.

Kampuni ya Simu Tanzania TTCL ipo mbioni kuanzisha huduma ya kusafirisha fedha kwa njia ya Mtandao ifikapo robo ya pili ya mwaka huu ili kutekeleza ombi la muda mrefu la Wateja wake wanaohitaji sana kuanzishwa kwa huduma hii kutokana na Mtandao mpana wa Kampuni uliosambaa ndani na nje ya nchi na unafuu wa gharama.

Popular Posts

Labels