Kampuni ya usalama mtandaoni ya SplashData imetoa orodha ya nywila au maneno ya siri yaliyotumiwa sana na watu mwaka uliopita.
Mwaka huu, neno ‘Star Wars’, kutoka kwa mwendelezo wa filamu za Star Wars, lilikuwa miongoni mwa maneno 25 yaliyotumiwa zaidi. Filamu ya Star Wars: The Force Awakens ilizinduliwa mwezi Desemba.
Wengi bado wanatumia ‘123456’ kama nywila na wengine ‘password’.
Ili kuwa salama mtandaoni, huwa ni vyema kutumia nyila ambayo watu wengine hawawezi wakaifikiria au kugundua kwa urahisi.
Moja ya njia za kuimarisha neno la siri ni kuchanganya tarakimu, herufi na alama pamoja na kuchanganya herufi kubwa na ndogo.
Lakini wengi hutatizika katika kukumbuka nywila.
Moja ya njia unazoweza kutumia ni kuangalia maneno ya wimbo uupendao na kuyafupisha.
Hapa kuna mfano wa jinsi unaweza kupata nyila kutoka kwa wimbo.
- Chagua mwanamuziki umpendaye, tuseme
- Chagua wimbo wake
- Tafuta mstari mmoja, sana ukupendezao zaidi,
- Fupisha kwa kuchukua herufi ya kwanza ya kila neno, au herufi mbili za kwanza. Tukichukua herufi mbili za kwanza.
- Changanya herufi kubwa na ndogo
- Kisha, badilisha herufi zinazokaribiana na tarakimu kuwa tarakimu, mfano badala ya ‘a’ tumia ‘@’ na badala ya ‘i’ tumia ‘1’.
Nywila zilizotumiwa sana 2015
Chanzo:BBC