Wednesday, November 25, 2015

VIKAO KAZI KWA WATENDAJI WA UMMA NCHINI TANZANIA SASA KUFANYIKA KWA KUTUMIA TEKNOHAMA



 

Serikali ya Tanzania  kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais imesema haitagharamia gharama zozote za kuendesha vikao kazi na watendaji wake kuanzia sasa, badala yake vikao hivyo vitaendeshwa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKINOHAMA). 

Wahusika wakuu wa vikao kazi hivyo ni pamoja na Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Florence Temba, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa, kupitia utaratibu huo washiriki wa vikao hivyo watabaki katika maeneo ya kazi ambapo wataunganishwa na mtandao wa pamoja kwa mfumo wa kuonana na kuongea uso kwa uso.

Aidha amewatoa hofu watumishi Kuhusu miondombinu ya mawasiliano kwa kusema Mfumo huo ni salama hakuna haja ya kuhofia kuhusu kukatika kwa umeme au hali ya hewa kwani mpango huo unaratibiwa na serikali hivyo ikitokea hali kama hiyo kutakuwepo na umeme wa ziada au kwa kutumia mkongo wa Taifa wa mawasiliano.

Popular Posts

Labels