Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) inatarajia kuzindua kituo kikubwa cha kuuzia intaneti Afrika Mashariki mwishoni mwa mwezi julai au Agosti mwaka huu.
Kituo hicho kinatarajiwa kuuza intanet mpaka nje ya nchi,ikiwa ni pamoja na nchi za Malawi,Rwanda,Burundi,Uganda pamoja na nchi nyingine jirani.
Hayo yameelezwa na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni hiyo,Peter Ngota,baada ya kupokea tuzo ya kampuni bora ya mawasiliano.
Amesema kuwa kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa huduma za intaneti ambazo zinawezesha upatikanaji wa huduma za matibabu mtando ambayo yanafanyika katika hospitali mbalimbali nchini.