Benki ya CRDB imewaonya wateja wake kuwa makini na baadhi ya mitandao inayoibuka na kulaghai kwa kuwataka wananchi,kutoa taarifa zao muhimu za kibenki,jambo ambalo linahatarisha usalama wa fedha zao zinazohifadhiwa na benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB,Dr Charles Kimei amesema jijini Dar es salaam hivi karibuni kuwa kumeibuka mchezo kwa baadhi ya mitandao ya kijamii,ikijaribu kuwalaghai wateja kwa kuwaomba taarifa za akaunti zao ili kufanya uhalifu.
Amesema wananchi wanatakiwa kuwa makini na kundi hilo,wasikubali kudanganyika kwa kutoa taarifa zinazohusiana na nyaraka nyeti za benki zao na kusisitiza kuwa ni marufuku kutoa taarifa hizo kwa wafanyakazi wa benki.
Mkurugenzi huyo amesema pamoja na kwamba benki hiyo inawapigia simu wateja wao wakitaka kukamilisha usaili wao kuhusiana na kuingia katika mfumo wa uboreshaji wa huduma za benki hiyo kupitia simu za mkononi unaoitwa Simbaking watambue kuwa hawataulizwa kutoa taarifa zozote za akaunti.
Kuhusu mbinu zinazotumiwa na wahalifu,Mkurugenzi wa Idara Hatarishi James Mabula amesema huwapigia simu wakijifanya kuwa wakurugenzi ama wafanyakazi wa benki hiyo na kisha kuwaghilibu kwa kutaka kupatiwa namba za siri za akaunti husika.
Popular Posts
-
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeingilia kati wizi wa fedha kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM), ambao umeibua hofu kubwa katika s...
-
Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katika hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana jijini Johan...
-
Upungufu wa usalama wa herufi za siri za takriban simu milioni 900 umewapa wadukuzi fursa ya kudhibiti simu za android kote duniani...
-
Wabunge wa Tanzania wameibana serikali wakiitaka iboreshe muswada wa sheria ya mifumo ya malipo ili kuzibana kampuni za simu na mabenki,kuto...