Jeshi la Kujenga Taifa JKT limekanusha taarifa zinazosambazwa
kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za
mkononina mitandao ya jamii kwa madai ya
kuwa vijana wanaofanya mafunzo ya katika makambi ya JKT wanapoteza maisha.
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Kanali Erick Komba amesema taarifa hizo si za kweli na
zina lengo la kupotosha vijana na watanzania kwa ujumla.
Luteni Kanali komba amesema kifo kilichotokea cha kijana HonorathaValletine
Oiso aliyefariki katika kikosi cha JKT Oljoro
mkoani Arusha kilitokana na upungufu wa damu na ugonjwa wa malaria,na si
kwa mafunzo ya kijeshi kama ilivyosambazwa kwa njia ya upotoshaji kupitia
mitandao.