Chuo Kikuu
cha Nelson Mandela cha jijini Arusha kimeanza utaratibu kuwashirikisha watafiti na wabunifu kutoka makundi mbalimbali katika jamii ilikukabiliana na tatizo
la Udukuzi wa taarifa za watu kwa vifaa vya mawasiliano vinavyotumia teknolojia mpya ya habari na mawasiliano.
Mkrugenzi wa chuo hicho Bwana Balton Mwamila amesema kuwa ilikufanikisha maadhimio hayo wameamuakuandaa maonesho ya
ubuni fu na ugunduziwa teknolojia inayohusu masuala ya kisayansi.
Amesema kuwa bado yapo matatizo yanayo ikabili jamii hasa
pale kunako tokea mabadiliko ya kisayansi huku kukiwa hakuna sheria zinazotoa miongozo inayombana mtumiaji wateknolojia mpya hali inayosababisha mtu kuangalia
au kudukua taarifazawatu.
Ameeleza kuwakupitia mtandao watu hufahamu undani wa mtu hasa kupitia taarifa zilizohifadhiwa hali aliyoeleza kuwa si sahihi nani hatari kiusalama hasa kwa mwenye taarifa za mtu binafsi.
Aidha swala udukuaji wa taarifa
au mawasiliano ya mtu bila ridhaa yamekuwa yakilalamikiwa katika nchi mbalimbali ambapo hivi karibuni nchi
ya Uingereza na Ujerumani ziliilalamikia nchi ya Marekani kupitia kikosi chake cha kijasusi kwa kile walichodai kuwa wamedukuliwa taarifa mbalimbali za kimtandao huku nchi nyingi hasa zinazoendelea zikiwa hazina sheria za kuwabana baadhi
ya watu wanaotekeleza vitendohivyo.