Wizara ya mawasiliano sayansi na teknolojia imesema mkongo wa
mawasiliano nchini Tanzania umefanikiwa kupunguza gharama za mawasiliano kwa
watumiaji wachini ktk maeneo ambayo makampuni ya simu yameshindwa kuyafikia.
Akizungumza na waandishi wa habarI
jijini Dar es salaam msemaji mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi
amesema mkongo huo unasaidia jamii ambapo huduma zinazohitaji viwango vikubwa
vya njia ya mawasiliano kama Elimu Mtandao, Biashara Mtandao, Afya mtandao,
mikutano mtandao zinapatikana kupitia mkongo huo.
Bi Ulomi amesema mkongo huo
umejengwa kwa viwango vya hali ya juu vya kimataifa na kuongeza kuwa kupitia
kifaa hicho Tanzania imekuza mahusiano nanchi jirani za Rwanda, Burundi,
Zambia, Malawi ,Uganda na Kenya kwani makampuni ya simu nchini Tanzania yametumia
mkongo huo kuunganisha nchi hizo.
Ameongeza kuwa mkongo
huo wa kimataifa ulioenea ktk maeneo mengi hapa nchini pamoja na nchi jirani
ktk awamu ya kwanzana ya pili utasaidia kufikisha huduma kwa wananchi kwa unafuu
na kuhakikisha maendeleo ya taifa kwani wananchi watapata fursa ya kutumia
Tehama ktk juhudi za kupambana na umasikini hapa nchini.