Friday, September 19, 2014

TEKNOLOJIA YA HUDUMA ZA KIBENKI KUPITIA M-PESA YAANZA KUTUMIKA ULAYA


The M-Pesa mobile money transfer system allows clients to send cash with their telephones (Reuters)
Picha kwa Hisani ya (Reuters)
 
Kwa muda mrefu nchi za Afrika zimekuwa zikitegemea teknolojia zilizobuniwa na kuundwa kutoka nje ya bara hilo,Kwa sasa teknolojia ya huduma za kibenki kupitia simu za mkononi iliyobuniwa na kuanza kutumika nchini humo imeanza kutumiwa barani Ulaya.

Teknolojia ya Huduma za kibenki kwa kutumia simu za mkononi ya M-Pesa ambayo inampatia nafasi mteja kutuma pesa kupitia simu mkononi imeonesha namna biashara inavyofanyika katika nchi za Afrika Mashariki na sasa imeanza kushika kasi katika matumizi yake nchini Romania.

Afisa wa Kampuni ya Vodafone nchini Kenya ameliambia shirika la Habari la AFP  hivi karibuni jijini Nairobi kuwa nchin zingine duniani zinapaswa kutazama matumizi ya huduma za M-Pesa kwani kuna mambo ambayo yanaweza kuchukuliwa toka nchi zinazoendelea na kupelekwa katika nchi zilizoendelea.

Huduma ya M-Pesa  ilianza kutumika  nchini Kenya mwaka 2007 na kampuni ya mtandao  wa simu ya  Safaricom ambayo ni kampuni ya simu kubwa nchini humo yenye ushirikiano wa kibiashara  na kampuni ya simu ya Vodafone ya nchini Uingereza ,

Nchini Kenya huduma ya M-Pesa imekuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ikiwa na wateja milioni 18 ikitumiwa na therusi mbili ya wakazi wa nchi hiyo huku ikihusisha mzunguko wa zaidi ya milioni 8 kwa siku.

Huduma hii huhusisha njia za kibenki kwa kutumia program tumishi inayopatikana kwa urahisi kwenye  simu za mkononi kwa kufanya malipo ama manunuzi ya bidhaa mbalilimbali au kutuma pesa kwa jamaa,ndugu,marafiki na wazazi.

Romania ni nchi ambako kampuni ya Vodafone imenza kuwekeza katika huduma zake za M-Pesa ikiwa ni nchi ya kwanza toka huduma hiyo ianze nchini humo mwezi machi mwaka huu ikihusisha malipo kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Michi Carstoiu,mhandisi toka mji mkuu wa Romania  Bucharest anasema huduma hiyo ni nzuri inaokoa muda na inatozwa gharama kidogo kwa mtumiaji

Barani Afrika huduma ya M-Pesa kwa sasa inatumia  Misri,Lesotho,Msumbiji na Tanzania na imeanzishwa hivi karibuni nchini India.


Popular Posts

Labels