Wakaazi bilioni 4.2 wa dunia hawana njia ya kutumia mtandao wa Intaneti.
Idadi hiyo ni sawa na asili mia 60 ya wakaazi wa dunia-benki kuu ya dunia imesema hayo mjini Washington.
Kumeibuka "pengo la digitali" kutokana na ule ukweli kwamba intanet inakutikana zaidi katika nchi tajiri.
Nchini India watu bilioni moja nukta moja hawana mtandao wa intaneti,nchini China wanafikia watu milioni 755 na Indonesia watu milioni 213.
Pengo hilo linazidi kuwa pana linapohusika suala la intaneti ya haraka-inasema benki kuu ya dunia.
Wanaofaidika na intaneti kama hiyo ni watu bilioni moja nukta moja tu-ikimaanisha chini ya asilimia 15 ya wakaazi jumla wa dunia.
"Watu wanabidi wajiepushe isiibuke "tabaka mpya ya wanaobaguliwa kijamii" anaonya mwanauchumi mkuu wa benki kuu ya dunia Kaushik Basu katika ripoti yake iliyopewa jina "Faida ya teknolojia ya habari."