Wapiga kura 2,845,256 wameandikishwa
katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi
wa mwili wa binadamu wa Biometric Voters Registration (BVR), mkoani Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, wapiga kura
hao ni sawa na asilimia 101.2.
Dar es salaam inaelezwa kuwa na wakazi wapatao 4,364,541 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.
Dar es salaam inaelezwa kuwa na wakazi wapatao 4,364,541 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.
Jaji Lubuva ametaja idadi ya walioandikishwa
katika wilaya za jiji hilo hadi Agosti 04 mwaka huu na idadi yao
kuwa ni Kinondoni 1,157,142 sawa na asilimia 105 wakati makadirio yalikuwa ni
watu 1,101,565,Temeke lengo lilikuwa watu 896,142, lakini walioandikishwa ni
886,564 sawa na asilimia 98.9 wakati Ilala lengo lilikuwa 811,716, lakini walioandikishwa ni 886,564 sawa na asilimia
98.9.
Kwa mujibu wa Jaji Lubuva, uwekajiwazi
wa daftari la kudumu la wapigakura kwa mikoa iliyokwishapokea daftari utaanza
Agosti saba na utadumu kwa siku tano.
Amesema lengo la uwekaji wazi huo ni
kutoa fursa kwa wale wote waliojiandikisha kusahihisha taarifa zao, kuhamisha
taarifa za wapiga kura waliohama toka kata au jimbo kwenda kata au jimbo jingine kutoa kadi kwa wapiga kura
waliopoteza kadi zao, kuangalia iwapo taarifa za mpiga kura aliyejiandikisha
zipo kwenye daftari na kuweka pingamizi kwa jina au taarifa za mpiga kura asiye
na sifa ya kuwamo katika daftari.