John Sculley aliyewahi kuongoza
kampuni ya Apple kwa muda wa miaka 10 (muongo mmoja) tangu mwaka 1983 amezindua
simu yake ya kisasa ya Obi Worldphone ambayo inatarajiwa kufanya vyema sokoni
hivi sasa na inatarajiwa kuwa sokoni rasmi hivi karibuni.
Simu
hii iko katika muundo wa aina mbili SF1 na SJ1.5
Aina ya simu hizi zimeundwa
kwa ushirikiano na studio ya ubunifu ya Ammunition iliyoko San Francisco,Marekani iliyoanzishwa na aliyekuwa Mkurugenzi
wa ubunifu wa kampuni ya Apple Robert Brunner.
Simu hizo zilizounda kwa
mfumo endeshi wa Android 5.1 zinateknolojia
ya kutumia simcard mbili zenye uwezo wa 4G
SF1 |
Ina 64-bit Snapdragon 615 processor ina uwezo wa 32 GB yenye RAM ya 3GB
huku ikiuzwa kwa dola 249 au yenye 16 GB na RAM ya 2 GB ikiuzwa dola za
kimarekani 199 na ikiwa na slot ya kuweka microSD kuanzia uwezo mdogo hadi GB
64.
SFI ina kamera ya nyuma yenye
uwezo wa -megapixel 13 inaweza kupiga picha bila kutoa mwanga ama kutoa mwanga
wakati kamera ya mbele ina megapixel 5
SJ1.5 |
Hii ni ndogo kuliko ile ya SF1 ina urefu wa nchi tano ina
prosesa ya 1.3 GHz
Ina memory ya ndani ya 16 GB na RAM ya 1GB na slot and supports microSD kuanzia ya chini
kabisa mpaka 32GB. Kamera ya nyuma
inauwezo wa kupiga picha kwa megapixel 8
na kamera ya mbele megapixel 5.
Obi Worldphone sio jina la biashara la kampuni jipya bali
lilianza mwaka 2014 kwa kutumia jina la Obi Mobiles ambapo ilijaribu kuuza simu
zilizoundwa toka China na kuuzwa huko India na Uarabuni.
Ukosefu wa kutofautisha na uhafifu wa ubora wa matoleo ya
simu hizo walifunga biashara ya simu huko India mapema mwaka huu.
Simu hizo zitakazokuwa katika mwonekano wa aina mbili tofauti na zenye rangi
nyekundu,nyeupe na nyeusi zinalenga kuwavutia vijana katika nchi za Asia, Afrika na Mashariki ya Kati.
Simu za Obi zitaanza kupatikana mwezi Oktoba katika nchi za
Vietnam, Indonesia, Thailand, Umoja wa Nchi za Kiarabu, Saudi Arabia, Kenya,
Nigeria, Tanzania, Afrika Kusini, Pakistan, Uturuki na India.
Watafiti wa masoko ya simu wanaeleza kuwa itakuwa jambo la
kuvutia kuona simu hizo za Obi zikiingia kwenye ushindani katika nchi za Asia
na Afrika ukilinganisha na kupotea kwa simu za Xiaomi, Honor na Motorola katika miaka iliyopita japo wanahofu
kuwa simu za Obi nazo zaweza zisifanye vyema kwenye soko la ushindani wa simu
za mikononi katika maeneo hayo.
.Angalia video hizi.