Monday, August 10, 2015

FACEBOOK,TWITTER NA GOOGLE KUONDOA PICHA ZA UTUPU ZINAZOWADHALILISHA WATOTO



Programu ya Swetie inayowatambua watu wanaowadhalilisha watoto kingono

Kampuni kubwa zaidi duniani za mitandao ya kijamii Google,Facebook na Twitter zimekubaliana kuondoa picha za utupu katika mitandao yao.

Hii inafuatia kuenea kwa picha za utupu za watoto kwenye mitandao ya kijamii.

Mashirika hayo kwa ushirikiano na shirika la kijamii linalopigania haki za watoto 'Internet Watch Foundation' (IWF) sasa yameanza kuorodhesha picha za utupu wa watoto kwa nia ya kuziondoa.

Wakitumia mbinu mpya ya kufichua watu wanaoshiriki ngono na watoto , IWF inakusudia kukomesha kudhalilishwa kwa watoto.

Hata hivyo mbinu hiyo imekosolewa na wadau wa maswala ya mtandao wa intaneti ambao wanasema kuwa bado kuna mbinu fiche ya kusambaza picha hizo nje ya mitandao hiyo kubwa ya kijamii. 

Wakitumia mbinu mpya ya kufichua watu wanaoshiriki ngono na watoto wanalenga kuondoa mamilioni ya picha za utupu wa watoto mitandaoni
Mwaka uliopita waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alionya kuwa shirika la kijasusi nchini humo litaanza ushirikiano na mashirika ya kijamii kukabiliana na kuenea kwa maeneo fiche kwenye mitandao ya intanet kwa nia ya kuwakamata watu wanaowadhalilisha watoto kingono.
Chanzo:BBC

Popular Posts

Labels