Na Yusuph Kileo
Nchi
ya Tanzania yabahatika tena kwa mara ya tatu kuwa mwenyeji wa mkutano
wa “Connect 2 Connect” ambapo kauli mbiu ya mwaka huu imekua ni
Kuunganisha bara la afrika mwambao hadi mwambao. Katika hotuba
iliyotolewa siku ya kwanza katika ufunguzi wa mkutano huo ili elezea
changamoto kubwa za usalama mitandao na namna unavyoweza kuleta athiri
kwa kiwango kikubwa endapo usalama huu mtandao hautaangaziwa macho.
Hotuba hiyo pamoja na mjadala nilio ongoza kwa siku ya kwanza unaweza
kusomeka na kuonekana kwa “KUBONYEZA HAPA”.
Mkutano
huu wa mara hii uliokusanya washiriki kutoka katika mataifa 30 duniani
kote ulihusisha wafanya maamuzi ya juu, watengeneza sera na wadau
wengine kadhaa ambapo Mawaziri na Manaibuwaziri wa Nchi kadhaa wkiwa ni
miongoni mwa waliopata kuongoza mijadala pamoja na kuunganisha mawazo
katika maswala mbali mbali ya barani Afrika.
Kongamano
hili la mwaka huu lililoandaliwa kwa kushirikiana wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia pamoja na kampuni ya simu ya TTCL
limeonyesha mafanikio makubwa sana kwa kuwezesha kauli mbiu ya mwaka huu
kufikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia mijadala mbali mbali iliyo jadiliwa
katia kongamano hili.
Mbali
na mada nyingine mbai mbali – Kwa siku zote mbili za mkutano huu
mijaadala mizito ya usalama mtandao ilipata kujadiliwa kwa kina ambapo
nilipata bahati ya kuongoza mjadala wa siku ya kwanza na kuhutubia kwa
siku ya pili juu ya maswala ya usalama mitandao.
Katika
hotuba yangu ya siku ya pili katika mkutano huu nilipata kuangazia hali
ilivyo duniani kote na kueleza kwa kifupi kuhusiana na Mkutano mkuu wa
mwaka ulioangazia maswala ya usalama mitandao jijini Johannesburg ambapo
pia nilihutubia kwa niaba ya Bara la Afrika tulipo kutana wataalam wa
maswala haya katika ngazi ya dunia. Zaidi niliweza kuainisha mapungufu
makuu tuliyo nayo yanayo sababisha vita dhidi ya uhalifu mtandao
kuenekana kutushinda kutokana na uhalifu huu mtandao kuendelea
kushamiri.
Msisitizo
mkuu niliotoa mbali na kuhimiza ushirikiano na kutumia vizuri wenye
ujuzi na elimu hii ya usalama mitandao, Nilipata kuainisha makundi ma
nne ambayo ni Mtu binafsi, kundi la Watu ( Wana usalama mitandao),
Kampuni , pamoja na serikali na kueleza kuna dhana potofu inayo dhani
makundi matatu kati ya hayo manne ndio yenye dhamana ya usalama mtandao
na kusahau kabisa kua lazima usalama mtandao uanzie katika ngazi ya MTU
BINAFSI.
Nikitolea
hili ufafanuzi – Nilielezea mtu binafsi anakila sababu ya kuhakiki
usalama wake uko vizuri kwa kuhakiki neno la siri “Password” Matumizi ya
salama ya mitandao na kuhakisha kila hatua za kujilinda dhidi ya
uhalifu mtandao kama ilivyo katika hali ya kawaida ya kulinda makazi
yetu zina angaziwa vizuri kwani jukumu la kulinda usalama mtandao si la
kundi flani la watu pekee.
Nikiwa na waziri wa TEKINOHAMA - BURUNDi |
Waziri
wa TEHAMA wa Burundi katika mazungumzo yake mkutanoni na baadae tulipo
kutana kwa mazungumzo baina yetu alionyesha dhahiri matumizi mabaya ya
mitandao hasa hii ya kijamii ilivyo changia kuyumbia taifa la Burundi
huku akiendelea kutoa wito juu ya matumizi salama ya mitandao ya kijamii
ili kuweza kuchochea usalama wa taifa lolote duniani – Katika kuumunga
mkono nilimpatia mifano kadhaa ya Nchi kama Misri, Libya na nyinginezo
ambazo ziliyumba na kuanguka huku sababu kuu ikiwa ni mitandao ya
kijamii kuchochea fujo katika nchini hizo.
Niliwa na Waziri wa TEKINOHAMA - LETHOSO |
Nilifarijika
kuona Nchi ya LETHOSO pamoja na NAMIBIA kuonyesha dhamira yao ya dhati
ya kutaka kujifunza kutoka kwetu kwenye maswala haya ya usalama mitandao
na kupongeza hatua nzuri tuliopiga hadi leo. Katika mazunungumzo yangu
na Waziri wa TEHAMA wa LESOTHO alinieleza wimbi kubwa na matumizi mabaya
ya mitandao nchini mwake ndio limeendelea kua kikwazo na ana mikakati
ya kuandaa sera pamoja na sheria mitandao ili kuhakiki ana himili
vishindo vya ukuaji wa matumizi mabaya ya mitandao.
Aidha,
Kwa upande wa NAMIBIA – Mbali na kunipongeza walionyesha dhamira ya
yadhati ya kufanyia kazi ushauri niliotoa katika mkutano huu, huku
wakisisitiza kua wanaamini kabisa tatizo kubwa ni upungufu wa ukuzaji wa
uelewa juu ya mambo ya usalama mitandao pamoja na serikali nchini
afrika kutoona Usalama mitandao ni kipa umbele na wakisahau Uhalifu
mtandao unauwezo mkubwa wa kuangusha taifa lolote.
Mwisho, Nitoe wito kwa serikali ya Tanzania na wadau mbali mbali kutambua athari kubwa katika Nyanja zote kuanzia kiuchumi hadi kisiasa zinazoweza kuonekana kama usalama mtandao hauta angaziwa macho ipasanyo. Wakati huu tukiwa tunaelekea uchaguzi mkuu lazima tujue mitandao ya kijamii inaweza kabisa kuyumbisha taifa letu hivyo hakuna budi kuwa na umakini madhubuti katika hili. Tayari nimesha lizungumzia hili mara kadhaa na zaidi unaweza kupitia Andiko linalosomeka kwa “KUBOFYAHAPA”