Imeelezwa kwamba kadri teknolojia inavyoongezeka, inatengeneza fursa ya
kukua kwa Shirika la Posta Duniani.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Shirika la Posta nchini, Fortunatus
Kapinga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Teknolojia.
Kapinga amesema kuwa teknolojia
inaleta fursa na sio tishio ila inategemea imetumiwaje katika eneo husika na
kuongeza kuwa biashara ya mtandao imeimarisha biashara ya shirika hilo ikiwa ni
pamoja na kutoa teknolojia mpya.
Aidha amesema kutokana na kuongezeka kwa biashara ya mtandao barani
Ulaya, mapato yamekuwa kwa asilimia 1.4, Asia na Amerika ya Kaskazini asilimia
3.9 na ameongeza kwa kusema kuwa shirika limefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali
ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Teknohama) ili kuongeza ubora
wa huduma zake.