Sehemu ya mji wa Gujarat ambako anatoka Waziri Mkuu wa sasa wa India Narendra Mod |
Jamii ya Patel walituma ujumbe mfupi wa maneno kwa raia kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kutosababisha machafuko katika eneo hilo.
Ujumbe huo umekuwa ukiambatanishwa na picha za video na sauti kupitia mtandao huo
Afisa mmoja wa Polisi amesema kuwa walikuwa wakifuatilia taarifa kuwa watu wamekuwa wakiwasiliana kuhusu suala hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp ingawa ametoa taarifa kuwa huduma za intaneti zitarejea baada ya kuwa wamejiridhisha na hali ya utulivu kama kawaida katika eneo hilo.
Taarifa zingine zinaeleza kuwa mawasiliano ya intaneti kwa njia ya simu yamezuiwa katika jimbo lote la Gujarat.