Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya kati imewataka watangazaji wa radio, luninga na mitandao ya kijamii kuwa makini na habari wanazotoa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais.
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa TCRA
Kanda ya kati, Maria Sasabo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye
maonyesho ya wakulima na wafugaji nanenane yanayofanyika katika viwanja vya
Nzuguni mjini Dodoma.
Amesema vyombo vya habari nchini vinatakiwa kutoa
haki sawa kwa pande zote mbili ili kuepusha mgongano wa kimaslahi unaoweza
kujitokea kwa kutangaza habari za upande mmoja.
Kwa upande wa wananchi waliotembelea
banda hilo walitoa akiwemo bwana Elieshiwakwe Malima amesema malalamiko yao
kuhusiana na baadhi ya mitandao kuwatumia ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu
zao za mikononi bila ridhaa yao.
Aidha Malima ameiomba TCRA
kuwadhibiti watangazaji hao na ikibidi wawe wanatumia namba zinazofahamika ili
kama kuna mtu anataka kujitoa kwenye huduma hizo aweze kutumia namba husika
kujitoa.