Thursday, August 20, 2015
GOOGLE WAZINDUA SIMU YA KISASA YA BEI RAHISI KWA AJILI YA AFRIKA
Google imezindua simu ya kisasa ya bei rahisi barani Afrika.
Simu hiyo, Hot 2 ambayo haina 'makorokoro' mengi itaanza kupatikana katika nchi sita za Afrika.
Itagharimu kati ya dola 85 na 100. Licha ya kuwa si watu wengi watakuwa na uwezo wa kuinunua, lakini ni bei rahisi kulinganisha na iPhone ambayo inauzwa hadi dola 1,000.
Uzinduzi huu ni juhudi za Google kujaribu kulikamata soko linalokua kwa kasi la simu za kisasa, ambapo watumiaji wengi bado hawana uwezo wa kuwa na vifaa vinavyoweza kuuganishwa kwenye mtandao wa internet.
Hot 2 imeshaanza kuuzwa na baadhi ya wafanyabiashara wa Nigeria na pia inapatikana kwa kununua kwenye mtandao kwa kiasi cha Pesa za Nigeria Naira 17,500 sawa na dola 88 na itapatikana pia hivi karibuni katika nchi za Ghana, Ivory Coast, Kenya,Misri na Morocco.
Kwa mujibu wa Google takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya wanaigeria milioni 50 wanaotumia intaneti asilimia 95 kati yao wanatumia simu za mikononi.
Simu hiyo ambayo ipo katika rangi nyeusi,,nyekundu,nyeupe,dhahabu na blue ina prosesa ya quad-core MediaTek yenye memory ya 16GB na inauwezo wa kutumiwa na sim card mbili,ikiwa imeundwa kwa program endeshi ya Android 6.0 Marshmallow