Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katika
hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana jijini Johannesburg mbali na mambo mengine
nilihimiza sana ushirikiano baina yetu kwani wahalifu mtandao wameendelea kua
mbele yetu kutokana na ushirikiano mkubwa waliokua nao. Ushirikiano unao
mabatana na kusambaza vitendea uhalifu mtandao bure auu kwa gharama nafuu
mitandaoni.
Baada ya kulizungumza hili laushirikiano wazungumzaji wengine
wote walionekana kuniunga mkono na hatimae kuonekana ni swala muhimu
lakufanyiwa kazi mapema. Nafarijika kuona Uingereza tayari mukuu wake wa CERT
ametilia mkazo kauli hii (Ya ushirikiano) kupitia kikao kilicho malizika London
ambapo taarifa kamili kuhusiana na hili inaweza kusomeka kwa “KUBOFYA HAPA”
Aidha, Marekani na Israel baada ya kutia saini makubaliano ya
kuboresha ushirikiano katika maswala ya usalama mitandao paliambatana na
kuhimiza mataifa mengine kuona umuhimu wa kushirikiana katika vita hii ya
uhalifu mtandao.
Nilipata kuzungumza tena katika mkutano wa wanausalama Nchini
Cyprus ambapo pia nilizungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na ushirikiano huku
nikipongeza umoja wa ulaya kwa kuungana kwao katika hili la usalama mitandao
kupitia chombo chao kiitwacho ENISA kinacho hudumia mataifa yote yaliyo ndani
muungano wa nchi za ulaya katika maswala ya Usalama mitandao.
Tayari kume endelea kuonekana jitihada mbali mbali zikifanyika
kupitia majukwaa yetu ya kimtandao ambapo tunajadili mambo mbali mbali na kuu
limekua kukumbushia ushirikiano huku wengi wakionekana kuelezea wazo hili la
ushirikiano nililo litoa mkutanoni limeendelea kusikilizwa na mataifa makubwa
huka mataifa mengine yakihamasishwa kuiga mfano.
Tanzania kumekua na Kauli kama Umoja ni nguvu, Kidole kimoja
hakifunji chawa, Umoja ni ushindi na nyinginezo zinazo hamasisha ushirikiano
katika nyanja mbali mbali lakini katika hili la kuunganisha nguvu katika
maswala ya uthibiti wa uhalifu mtandao bado naona safari ni ndefu.
Nalisema hili kwa sababu bado uhalifu mtandao unaendelea
kukua na ki uhalisia vitengo vinavyo husika na hili nchini bado vimekua
havionekani kuungana na kua na uwezo mmoja madhubuti kwa kuhimili uhalifu huu.
Kuungana ninaotegemea mimi ni pamoja na kushirikiana katika taarifa, Vitendea
kazi pamoja na wataalam ambapo kwa ujumla wake yote matatu yame gawanywa
inayopelekea kuto onyesha matunda tegemewa.
Nitatolea mfano uhalifu mpya uliokuja kwa kasi nchini na
wengi wamonekana kuathirika huku athari ya uhalifu huu baada ya kujaribu
kujadiliana na wngine wameweza kueleza athari kubwa ipo kwa Tanzania na isipo
angaziwa baadae inaweza kuibua uhalifu mwingine ambao utakua ni matunda ya huu
ulioko sasa na pengine kua na madhara makubwa sana kwa taifa kiujumla.
Nitoe wito katika hili kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii
kufahamu ya kua hawana buni kuhakiki wanaendelea kua na tabia ya kujijengea
ulinzi katika ngazi ya mtu binafsi mtandaoni huku wakiwa makini sana na
kutafakari sana kabla ya kuandika “THINK BEFORE YOU INK” huku umakini na
kubadilisha maneno ya siri kua ni moja ya tabia ya watumiaji mitandao kwani
neno la siri madhubuti na linalo badilishwa itakikanapo husaidia kuzuia uhalifu
wa udukuzi.
Matumizi salama ya mitandao ya kijamii na kutambua utumiapo
mtandao wa kijamii kusemea wengine vibaya au kutumia lugha zisizo rafiki kwa
wengine inasababisha uhalifu aina ya Cyberbulling ambao umeendelea kugharimu
sana uhai wa watu duniani kote.kuendelea kuangaza macho kwenye mifumo yetu yote
ya digitali pia ni muhimu sana kwani ukuaji wa matumizi ya digitali katika
maisha yetu lazima tujue yanakuja na changamoto za ukuaji wa uhalifu mtandao
hivyo hatuna budi kuongeza umakini katika usalama mitandao.
Na:Yusuph Kileo