Tuesday, November 1, 2011

ZANZIBAR YAZINDUA TEKNOLOJIA YA KUONGOZA VYOMBO VYA USAFIRI BABARINI

Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imezindua mfumo mpya wa kuongoza vyombo vya usafiri majini utakaotumia kompyuta kwa lengo la kuvifuatilia vikiwa njiani.

Teknolojia hiyo ya Digitali inayofanana na ile ya ndege, inaingia sokoni kukabiliana na ajali za meli zisizokuwa za lazima.Akizindua teknolojia hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, alisema mfumo huyo utasaidia kuwabana wafanyabiashara wote wasio waaminifu ambao wanaweka mbele maslahi yao na kusahau utu.

Hivi karibuni zaidi ya watu 1,000 wanasadikiwa kupoteza maisha kufutia ajali ya meli ya Mv Spice Islands, baada ya kuzama katika mkondo wa Nungwi kufutia boti hiyo kujaza mizigo kupita uwezo wake.

Kutoka: Gazeti la Mwananchi

Popular Posts

Labels