Friday, November 25, 2011

UNUNUZI WA T-MOBILE WAKWAMA

Makubaliano ambayo yangeiruhusu kampuni kubwa ya simu ya Marekani, AT&T kuinunua kampuni ya T-mobile tawi la Marekani la kampuni ya Ujerumani ya Telekom, yamekubwa na matatizo ya kawaida ya Marekani. Kutokana na hali hiyo kampuni ya AT&T imesema huenda ikachukuwa dhamana ya malipo ya dola bilioni 4, pindi ikishindwa kuinunua kampuni ya T-Mobile.

Wizara ya sheria na Tume ya mawasiliano ya Marekani zote zimepinga makubaliano hayo, ambayo pindi yangefanikiwa yangepunguza idadi ya  kampuni kubwa za simu za taifa kufikia tatu. Wapinzani wa mkataba huo wanasema utahujumu nafasi za ajira na kupana mashindano ya kibiashara. Kampuni ya AT&T na mmiliki wa T-Mobile, kampuni ya Deutsche Telecom, zinasema zitaendelea kutafuta njia za kuidhinishwa ununuzi huo utakaogharimu dola bilioni 39.
Kutoka: Deutsche Welle

Popular Posts

Labels