Wednesday, November 2, 2011

UNAITUMIAJE FACEBOOK???


Imeelezwa kuwa Idadi kubwa ya vijana wanatumia mtandao wa jamii wa Facebook ambao wengi ni wanafunzi wanakosa maadili baada ya kuutumia kwa kujinadi kwa kuweka picha za nusu uchi,hali inayodaiwa kuhatarisha maisha na mustakabali wao.

Gazeti la Majira katika kurasa zake za maisha lilifanya utafiti miezi mitatu ili kuona hatari hiyo ambapo liligundua kuwa vijana wengi wamekuwa wakitafuta wapenzi katika mtandao bila kujua tabia ya mtu unayemtaka.

Utafiti huo pia umebaini idaidi kubwa ya vijana waliojiunga katika mtandao huo ni wanafunzi wa Sekondari,Vyuo Vikuu wengi wakiwa na lengo la kutafuta wapenzi ambao hupatikana baada ya kuwasiliana nao na kuangalia picha.
Katika utafiti huo gazeti hilo lilizungumza na baadhi ya vijana katika mtandao huo ambapo walisema kuwa wamekuwa hawasumbuki kupata wapenzi kwani wengi wanaotumia mtandao huo wanaonekana ni watu wenye uwezo wa kifedha.
“Unajua humu ndani wanawake huwa wanaweka picha za nusu uchi ambazo kwa kweli huleta hamasa kwa mwanaume,lakini hata hivyo wengine walio na ufahamu mdogo,wanahisi kwamba wote walio katika mtandao huo ni wale waliojiweza kifedha kitu ambacho hakina ukweli wowote”alisema Mac Peter.

Alisema kuwa kwa kuwa upande wake amekuwa akitumiwa namba na wanawake kwa lengo la kutaka wazungumze kwa njia ya simu ambapo asilimia kubwa ni wanafunzi wa sekondari na vyuo.

Gazeti hilo pia lilizungumza na baadhi ya vijana wa kike ambao wanaweka picha za nusu uchi walisema kuwa wengine hutafuta wachumba lakini wengine huweka kwa lengo la kujifurahisha na kuweka mambo yao.

“Ni kweli wapo wanawake ambao wamejiweka humu facebook wanatafuta wanaume na picha zao walizoweka nyingi ni zile ambazo zinaonesha miili yao sasa sijui hao wanaume wanaowatafuta wanawajua,lakini mi naona ni hatari kwa sababu kuwa na mahusiano na mtu usiyemjua ni hatari”alisema Aisha.

Naye Kijana aliyejitambulisha kwa jina la Benedicto Julius  alisema kuwa anaamini kwa asilimia nyingi kwamba wanawake wanaoweka picha zinaonesha miili yao wanatafuta wanaume.

Hata hivyo aliongeza kuwa endapo vijana wangekuwa wanatumia mtandao huo kwa malengo yaliyokusudiwa badi hata uwekaji wa picha za ajabu usingekuwepo.

“Facebook imewekwa kwa ajili ya watu tuweze kuwasiliana na kutafuta marafiki pande zote za dunia,pia hata kuweza kufundishana baadhi ya mambo ambayo hatuyajui,lakini watu wengine wanafanya kinyume kwa kuutumia kama sehemu ya kujiuza na kuwa sehemu ya kupata wanaume na wanawake’alisema.

Hata hivyo mmoja wa wasanii walio katika mtandao huo Esther Flavian alisema kuwa wapo wanawake wengine ambao hutumia pesa nyingi kupiga picha za nusu uchi ili tu waweze kuziweka mtandaoni.

Alisema vijana wengi wanaofanya matendo hayo machafu ni wanafunzi hivyo wanakuwa katika hatari kubwa ya kuharibu sifa zao ambazo baadaye zinaweza kuwaletea matatizo.

“Unajua humu ndani kuna picha nyingine mtu unashindwa kuzielewa kwamba mtu unashindwa kuzielewa kwamba mtu anaweka hizi picha kwa manufaa ya wengine au kwa ajili ya kuonesha mwili wake ulivyo”alihoji msanii huyo

Popular Posts

Labels