Shehena ya Mizigo inayopitia bandari na mipaka ya Tanzania kwenda nchi za nje kuanzia mwakani itakuwa ikifuatiliwa kwa mfumo wa kielektroniki kuhakikisha kwamba inafika nchi husika lengo likiwa ni kudhibiti wanaokwepa kulipa ushuru.
Naibu Kamishna,Uboreshaji na Udhibiti wa Vihatarishi wa Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA,Bellium Silaa amesema kulingana na sheria za kimataifa kawaida mizigo inayotolewa bandarini kwenda nje ya nchi haitozwi ushuru.