Thursday, November 3, 2011

KAMATI YASEMA TCRA INA MATUMIZI MAKUBWA

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) nchini Tanzania imeshitushwa na matumizi makubwa ya fedha yanayofanywa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo (TCRA) kwa kufuja shilingi bilioni 600 za kitanzania.

Makamu mwenyekiti wa POAC  Deo Filikunjombe amesema kuwa hayupo tayari kupokea ripoti ya mamlaka hiyo kwa kuwa imejaa ufujaji mkubwa wa fedha.

Taarifa ya mamlaka hiyo inayosimamia mawasiliano nchini Tanzania imeonesha kuwa fedha nyingi hutumika katika semina na kozi mbalimbali ambazo hutolewa kwa wafanyakazi wake ambapo kwa mwaka jana zilitumika zaidi ya shilingi bilioni 4.1 za kitanzania kwa ajili ya mafunzo na semina wakati shilingi bilioni 3.3 zilitumika kuwalipa wafanyakazi posho zao ambazo hutolewa kwa wafanyakazi waofanyakazi kwa muda wa ziada.
Wajumbe wa kamati hiyo pia walihoji uhalali wa wajumbe wa bodi ya TCRA kulipwa posho na fedha za matumizi ya simu kila mwezi kwa zaidi ya Dola 2,800 za Marekani.
Filikunjombe amesema kuwa kwa kawaida Mkurugenzi Mkuu wa TCRA anapaswa kuwa na matumizi ya kawaida ya kuanzia shilingi milioni 10 hadi 50 lakini kwa hesabu za mamlaka hiyo zinaonesha wametumia zaidi ya shilingi milioni 600 bila kutoa mchanganuo unaoridhisha.

Kamati hiyo pia iliitaka TCRA kuonyesha mchanganuo wa fedha za tozo kwa kampuni za simu zinazofanyakazi zake nchini baada ya kushindwa kuwasilisha matumizi ya kampuni ya Vodacom na Zantel.
Filikunjombe alieleza kuwa kampuni ya Vodacom inaonekana imelipa kiasi cha Dola 600 za Marekani na Kampuni ya Zantel inaonekana imelipa Dola 160 za Marekani,lakini cha ajabu katika kumbukumbu za TCRA hakuna maelezo yanayojitosheleza kueleza pesa hizo zilipo.

Popular Posts

Labels