Thursday, December 1, 2011

TAHADHARI INTERNET INAUA NGUVU ZA KIUME

Habari si nzuri kwa wanaume wanaopenda kutumia wireless internet kwenye laptop zao wakiwa wameziweka laptop zao mapajani au karibu na viungo vyao muhimu vya kiume, utafiti wa wanasayansi wa Marekani na Argentina umeonyesha kuwa wireless internet inaua mbegu za kiume.

Utafiti uliofanywa na wanasayansi toka Marekani na Argentina umeonyesha kuwa wireless internet kwenye laptop ina madhara kwa viungo vya uzazi vya mwanaume kwa kuharibu ubora wa mbegu za kiume au kuziua kabisa.

Utafiti uliofanywa kwa kuweka mbegu za kiume chini ya laptop inayotumia wireless internet ulionyesha kuwa mbegu za kiume zilipungua ubora wake na hivyo kupunguza chansi ya mwanaume kupata mtoto.


Utafiti huo ulifanywa na timu ya wanasayansi toka taasisi ya Nascentis Centre for Reproductive Medicine iliyopo Cordoba, Argentina kwa kushirikiana na wanasayansi wa Marekani wa taasisi ya Eastern Virginia Medical School.


Mbegu za kiume za wanaume 29 wenye afya njema wenye umri kati ya miaka 26 na 45 zilikusanywa na kugawanywa makundi mawili. Kundi moja la mbegu za kiume liliwekwa chini ya laptop inayotumia wireless internet na jingine liliwekwa mbali na laptop zinazotumia wireless internet.


Matokeo ni kwamba robo ya mbegu za kiume zilizowekwa chini ya laptop yenye wireless internet ziliuliwa ndani ya masaa machache. Vinasaba au DNA ya mbegu za kiume nazo ziliharibiwa.


Kwa upande wa pili, mbegu za kiume zilizowekwa mbali na laptop hazikuonyesha kupatwa na madhara yoyote zaidi ya kupungua kidogo sana kwa spidi ya kuogelea ya mbegu za kiume.


Wakati huo huo, mbegu za kiume zilizowekwa chini ya laptop ambayo haikuwa imeunganishwa kwenye internet hazikuonyesha kukumbwa na uharibifu mkubwa kama uliotokea pale zilipowekwa chini ya laptop iliyounganishwa kwenye wireless internet.


"Utafiti wetu unaonyesha kuwa kutumia wireless internet huku ukiwa umeiweka laptop karibu na viungo vya uzazi hupelekea kuharibika kwa ubora wa mbegu za kiume", alisema Dr Conrado Avendano, ambaye ndiye aliyeongoza utafiti huo.


"Kwa sasa hatujui kama madhara haya yapo kwenye laptop zote ziliounganishwa kwenye wireless internet au la".


Sababu ya kuharibika kwa mbegu za kiume huenda ikawa inasababishwa na miale ya electromagnetic inayotolewa na wireless internet.


Matokeo ya utafiti huu yamewekwa kwenye jarida la mwezi huu la Fertility and Sterility journal, ingawa dokta Avendano amewataka wanaume wasipaniki kwani tafiti zaidi zinaendelea kuhusiana na suala hili.
Habari toka www.nifahamishe.com 

Popular Posts

Labels