Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ,Bw Charles Kitwanga ameyashawishi mataifa ambayo tayari yamejiunga na mfumo wa Digitali katika harakati za kuharakisha mawasiliano bora duniani kutumia nafasi hiyo kutoa ubunifu wao na ikiwezekana kuyasaidia yale ambayo ndiyo yanaanda ili waweze kufikia lengo la pamoja kwa wakati.
Changamoyo hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Arusha wakati akifungua mkutano wa sita wa Mamlaka za Mawasiliano wa nchi za Afrika (ACRAN) unaoshirikisha nchi zaidi ya 20 wanachama wa jumuia hiyo kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Bw Makame Mbarawa.
Kitwanga aliwataka wataalamu hao ambao nchi zao tayari zimeingia kwenye mfumo wa digitali kusaidia mataifa ambayo yanaelekea kujiingiza katika mfumo huo.
Tanzania hasi kufikia Disemba mwakani mashirika yote yanatakiwa yawe yanatumia mfumo wa digitali na kuachana na analogia hivyo ni wajibu wa wadau mbalimbali kuwaelimisha wananchi namna ya kutumia mfumo huo.
Mashirika ambayo yamepewa dhamani ya kuuza ving'amuzi ni pamoja na Star Times,Ting Agape TV, Sahara Communication na IPP Media