Miaka 10 iliyopita watu wengi walitumia search engines kwa ajili ya kutafuta vitu kwa njia ya mtandao zaidi ilikuwa ni viunganishi vya vitabu habari mbalimbali kuhusu watu au mambo wanayoyataka wao na wavuti nyingi za search engines zilikuwa na njia hiyo moja tu haikumpa mtu fursa zaidi kama akitaka ilibidi mpaka aingie kwenye wavuti husika .
Miaka 5 iliyopita kampuni za search engines duniani zilibadilika kwa kiasi kikubwa mpaka sasa hivi ambapo mtu unaweza kutafuta jambo Fulani na ukaamua kama unataka kuona picha yake tu au unataka nyaraka yake kwa mfumo wa pdf tu au mawasiliano tu na fursa nyingine nyingi kutumia mtandao .
Katika kipindi hicho cha miaka 5 iliyopita taasisi za elimu
ulimwenguni na kampuni mbalimbali ziliingia zaidi kwenye utafiti wa kufanya search engines ziweze kutafuta vitu maalumu kwamba sasa kuwe na search engines za vitu maalumu kama ni daktari aweze kutembelea search engine yenye vitu anavyotaka yeye na sio majibu anayotaka yahusiane na vile asivyotaka yeye .

Sasa hivi kuna search engine za vifaa vya magari tu kwa njia ya
mtandao , kuna pia za vioo tu aina mbalimbali za vioo , kuna search engine za kutafuta nyaraka za PDF tu au Nyaraka za Doc za Microsoft word tu na nyingine nyingi sana .
Pia wengine walifanya utafiti kuona wanavyoweza kutumia search engines na program nyingine za tarakilishi kuweza kutafuta vitu na kuvitambua katika muda mchache nap engine kupata taarifa zaidi kuhusu kitu hicho .
Mimi ni mmoja ya watu walioingia kwenye utafiti huu kwa kipindi hicho kwa kushirikiana na chuo kimoja pamoja na mashirika kadhaa ambapo kwa kiwango kikubwa sana nimeweza kupata majibu na kuweza kuendeleza mengi zaidi
SABABU KUU
Kilichonifanya kuingia kwenye shuguli hii ni Filamu ya Black Hawk Down
iliyokuwa inahusu shuguli za wajeshi wa marekani nchini Somalia .
Kuna tukio moja ambapo Helcopter ya Jeshi ilikuwa inataka kufanya
shambulio mahala lakini hawakujua haswa ni nani aliyekuwepo kwenye jengo hilo na wanajeshi waliokuwa ardhini hawakuweza kuonekana kilichokuwa alama yao kuu ni Gari yao wenyewe iliyokuwa ina alama juu ambayo ndio rubani wa helcoper aliangalia .
Hii filamu ni ya zamani kidogo lakini mpaka siku za karibuni majeshi na vyombo vingi vya usalama vimeshindwa kupata taarifa sahihi za mtu au kitu wanachotafuta matokeo yake ni kuumiza wengi zaidi na kuharibu mali .
Hata kwenye uvamizi wa jeshi la kesho nchini Somalia sasa hivi
kumeonyesha udhaifu huo huo wa kutopata taarifa sahihi kabisa kabla ya kufanya shambulio .
KILICHOFUATIA .
Kwa sababu nimekuwa kwenye Uendelezaji wa Programu za Google Earth na hii ndio ilikuwa nyenzo yangu muhimu kwa kushirikiana na Huduma nyingine za Kampuni la Google na Search engine tofauti na Mitandao mengine ya Jamii .
Google Earth bado ina huduma nyingine nyingi za kufanyia utafiti zaidi na kazi ili kuweza kupata bidhaa mbalimbali kama hii yangu
MATOKEO YAKE .
Kwa sasa hivi Tunaweza kupata halaiki ya watu zaidi ya alfu 6
waliokusanyika sehemu moja na kuweza kutambua sura za watu hao kisha kupata taarifa zao nyingine zilizohifadhiwa kwenye database katika kipindi kifupi sana kama mtu huyo alikuwa anatafuta kwa njia yoyote ile ni rahisi kupatikana kama alikuwa kwenye halaiki hiyo .
Kama kuna hatari zozote za mafuriko , moto na majanga mengine mfumo huu unaweza kutoa taarifa za kina kwa wadau mbalimbali na wataweza kuchukua hatua madhubuti za kudhibiti hali au hata kuwasiliana na wale waliochini.
HII NI KIFUPI KUHUSU MUELEKEO WA SEARCH ENGINES
Karibuni kwa maoni mbalimbali na maswali mbalimbali .
Sijaandika kitaalamu zaidi kuhusu kitu hichi ili watu waweze kuuliza maswali na nijibu lakini msiogope .
Yona Maro-+255786 806028 au oldmoshi@gmail.com