Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway
kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.
|
Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa
kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es
Salaam.
|
Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba
la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli
ya Serikali utakavyokuwa unatumika.
|
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa
kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo
nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.
Mfumo
huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa
ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa
GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa
kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka
kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Majaribio
ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki
yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa
kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika
Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa
mikoani.
Mwananchi
yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza
kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa
na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.
Kwa
zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile
upekuzi katika daftari la msajili (official
serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo
katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba
ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.
Kwa
sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza
kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es
Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji
wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi
nchini,