Dunia ya ulinzi na usalama wa masuala ya mawasiliano inapitia kipindi kigumu kwa kipindi cha miaka 5 sasa ambapo wahalifu wengi wamekuwa na ushindani wa kuiba taarifa mbalimbali kwa njia ya mtandao ili kuweza kuzitumia taarifa hizo kwa ajili ya shuguli mbalimbali kutegemeana na uhitaji wa taarifa hizo .
Katika dunia ya uhalifu kwa njia ya mtandao haswa unaohusu taarifa kuna makundi 5 yanayojulikana zaidi kutokana na nia zao za kuiba taarifa hizo .
Kundi la kwanza ni la wahalifu wa kifedha hawa wanaiba taarifa pale ambapo unaingiza taarifa zako kwenye mitandao usiyoijua taarifa hizo zinahifadhiwa sehemu fulani kwa ajili ya kutumika sehemu nyingine za dunia hawa mara nyingi wanahamisha fedha kwa kutumia taarifa walizopewa na mtu asiyejua vyema kile anachokifanya kwa njia ya mtandao .
Kukabiliana nayo Kuna benki zenye vifaa vinavyoitwa KeyChanger hiki ni kifaa unachokuwa nacho mkononi kama flashdisk au remote control pindi unapotaka kuingia kwenye akaunti yako ya benki kwa njia ya mtandao unabonyeza kifaa hicho na kupatiwa Password Mpya .
Sio benki zote zenye huduma hizi na mara nyingi inategemea na kiasi
cha hela ulichonacho kwenye benki husika yaani mteja wa aina gani .
Geo Location
Geo Location ni tabia za mtumiaji wa huduma za kibenki pale alipo ,benki nyingi hazina utaratibu za kujua tabia za mteja wao na
kumfuatilia pale anapochukulia hela mara kwa mara au tarakilishi
anayotumia kuingilia kwenye mtandao wa benki hiyo mara kwa mara
Benki zikianzisha Geo Location kwenye uchukuaji wa pesa ina maana kama mtu yuko Dar es salaam na amekuwa anachukulia pesa Dar es salaam tawi la Mlimani City kwa mfano akihamia Mwanza asiweze kutoa fedha kwa muda huo mpaka aweze kudhibitisha taarifa zake au mtu akiwa Kenya na kufungua akaunti hiyo hiyo asiweze kufanya hivyo bila kujibu baadhi ya maswali kwa mfano mara ya mwisho kutoa hela alitumia tawi gani tarehe ngapi .
Kundi la pili na ambalo linakuja juu zaidi ni uhalifu au uharamia wa mtandao kwa ajili ya kutafuta taarifa kuhusu Taifa fulani , vikundi fulani vya watu wanaotumia mitandao kuwasiliana zaidi mitandao jamii na wavuti za serikali za nchi wanazopingana nazo au za wanaharakati au vyama vya siasa labda upinzani au vinavyotawala .
Kukabiliana nayo
Kwa serikali na taasisi nyingine nyeti ni vizuri kuwa na programu na mifumo imara ya mawasiliano na kuwa na watu wa ulinzi na usalama kwa njia ya mtandao , pili ni kwa serikali na taasisi zake kufanya mabadiliko kwenye programu( customise ) wanazotumia katika tarakilishi zao ili ziweze kuendana na mazingira yao pamoja na mahitaji yao .
Nchi zilizofanikiwa zaidi kwa kubadilisha programu ni Umoja wa Ulaya ambao umeingia mkataba maalumu na kampuni zinazotengeneza programu hizo kama Microsoft , oracle ,Adobe ,Symantec
Kundi la tatu ni wale wanaoiba taarifa kwa nia tu ya kutangaza bidhaa zao au huduma zao nyingine kutumia anuani pepe haswa zile za bure kama yahoo ,hotmail hii imeathiri watu wengi wa nchi maskini haswa chini ya jangwa la sahara ambapo hawana uwezo mkubwa wa kukabiliana na baadhi ya vitu vipya kwenye teknologia .
Kukabiliana nayo
Kitu cha muhimu ni kwa watu kuacha kutumia barua pepe za bure sasa hivi kusajili rajisi Domain ni bei ndogo sana unaweza kusajili domain name yako kama www.mwanahawa.co.tz kwa ajili ya wakazi wa tanzania au www.mwanahawa.co.ke kwa wakazi wa kenya chochote kikitokea hapo unaweza kupata kwa urahisi kutoka kwa msajili wa rajisi hizo kwa tanzania ni www.tznic.or.tz
Kundi la nne ambalo sipendi kuliongelea sana ni wale wanaoiba na
kuzichapisha kwa nia ya kuharibu taswira ya mtu , mataifa , makundi mengine ya jamii haswa wale wanaopingana nao au wanaoona hawafanyi kazi vizuri na kuwajibika hawa wengi wako kwenye mitandao jamii kama wikileaks na zambiawatchdog .
Kukabiliana nayo
Hii ni ngumu kidogo maana inategemea taarifa zimetokea wapi kama ni Hardcopy au Softcopy kukabiliana na hali hii ni kutumia mifumo
endelevu ya digitali kwa ajili ya kuhifadhi taarifa kama ni kwa njia ya karatasi au kwa njia Mtandao na wafanyakazi wa sehemu nyeti kuchukuliwa alama zao za vidole na nyingine ili ziweze kutumika endapo taarifa zimevuja au kwenda kwenye mikono ambayo sio sahihi
Kundi la 5 ni mafundi au watumiaji wengine wa tarakilishi ambao
wanaweza kuiba taarifa zako kwa njia ya vihifadhi kama
flashdisk ,Cd ,au kama kuna mtandao wanaweza kuzirushia kwenye mtandao hapo hapo zaidi kuhusu mafundi wa tarakilishi ni pale unapopeleka kompyuta yako kwake kwa ajili ya matengenezo hapo taarifa zako zinaweza kuibiwa .
Kukabiliana nayo
Hakikisha Taarifa zako nyeti unaondoa kabla ya kupeleka kifaa chako sehemu za mbali kwa ajili ya matengenezo ingawa mtu ataweza kupata taarifa hizo kwa kutumia program nyingine za kurudisha taarifa hizo ( recovery ) njia bora zaidi ni kuwa na watu wako wa kurekebisha matatizo ya ufundi ambao una mikataba nao inayohusu uhifadhi wa taarifa ( data act )
Taarifa nyingi sana zimekuwa zikiibiwa na kutumika ndivyo sivyo na vyombo vingine lakini pia vyombo vingine havijachoka kubuni na
kutengeneza program mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mali za watu , suala lililo kuu kuliko yote ni kwa mtu mwenyewe , taasisi au serikali kuwafunzi wafanyakazi wake kuhusu taratibu nzuri za kuhifadhi taarifa na kuzitumia haswa kwa njia ya mtandao , kuwa na program nzuri za ulinzi na usalama ambazo ziko updated na wenyewe kupenda kutafuta taarifa na maarifa zaidi kuhusu ulinzi na usalama wa mali zao kwa njia ya mtandao .
Njia nyingi hapo kuweza kuzitumia sawa sawa ni gharama na zinahitaji uwekezaji haswa kwa muda mrefu kwa njia ya elimu ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhalifu huu .
YONA FARES MARO
DAR ES SALAAM
+255786806028