Udukuaji huo umetumia program ya udukuaji iliyotengenezwa na shirika la usalama wa taifa la Marekani (US National Security Agency-NSA) ambalo nalo lilibiwa program hiyo na wajanja.
Wadukuaji hao wanaojiita The Shadow Brokers ndio wanaodai kuwa waliiba program hiyo na kuiweka hadharani katika mitandao ya internet.
Kampuni ya Microsoft ilitengeneza ngao ya kuzuia udukuaji kwa kutumia program hiyo na kuiweka hadharani mwezi Machi, lakini ni wazi watu wengi hawakutumia nafasi kuweka ngao hiyo.
Kampuni mbalimbali kutoka nchi 99 zinasemekana mitandao yao imetekwa, kumekuwa na malalamiko kutoka Uingereza, Marekani, China, Urusi, Hispania, Italia,Taiwan na nchi nyingi nyingine.
Kampuni ya ulinzi wa mitandao (Cyber-security) ya Avast imesema imeweza kupata malalamiko 75,000 ya madai ya kuhusu kirusi cha WannaCrypt, kutoka karibu pande zote duniani.
Hivi ndivyo kompyuta inavyosomeka ukishadunguliwa na kirusi cha Wannacry |
Urusi imesema imeweza kugundua chanzo na inakishughulikia. Huko Ujerumani kampuni ya kuuza tiketi za treni imekubwa na kadhia hiyo wakati maabara ya chuo kikuu kimoja Italy imekutana na tatizo hilo.
Spain imejikuta ikipata tatizo hilo kwenye kampuni yake kubwa ya simu ya Telefonica, kampuni ya umeme ya Iberdrola na kampuni ya kusambaza gesi ya Gas Natural, wafanyakazi wa kampuni hizo walielekezwa kuzima kompyuta zote.
Kampuni ya simu ya Portugal Telecom, na kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx, ofisi moja ya serikali ya mtaa huko Sweden na kampuni ya simu za mkononi ya Megafon ya Urusi ni kati ya wahanga wa tatizo hili.
Nani hasa waliosababisha hili? Wataalamu wengine wanasema wahusika inawezekana waligundua mapungufu katika program ya Microsoft, NSA waliliona hilo pia na walitengeneza program iliyokuwa inaweza kuteka kompyuta zote zinazotumia Microsoft, program hiyoikaibiwa na wezi wanaojiita (The Shadow Brokers), wezi hawa walianza kuinadi program hiyo katika mtandao na hatimae tarehe 8 April 2017, wakaigawa bure kwa kusambaza password mtandaoni. Wakidai wamefanya hivyo kama njia yao ya kumpinga Rais Donald Trump.
Microsoft tayari wameshatengeneza program ambayo itakuwa inaweza kutoa taarifa kama kompyuta yako imeingiliwa na udukuzi wa WannaCrypt.
CHANZO:theiringa.blogspot.com