Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda |
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda amewasihi wadau wa elimu nchini Tanzania kujitokeza kuchangia uanzishwaji wa maktaba ya kielektroniki ili kuondoa mizigo ya ubebaji wa madaftari kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Pinda ametoa kauli hiyo huko Arusha jana alipokuwa akizindua mradi wa makataba za mkononi za kielektroniki katika shule mbili, za Nanganga na Nambala ambazo zimefadhiliwa na Chuo cha Nelson Mandela na Taasisi ya Worldreader ya Marekani iliyotoa vitabu hivyo vilivyohifadhiwa katika mfumo kama wa laptop ambavyo vinahifadhi zaidi ya vitabu zaidi ya 100 vya masomo mbalimbali