Wednesday, May 15, 2013
GOOGLE KUTANGAZA UTOAJI WA HUDUMA YA MUZIKI LEO?
Tovuti ya readwrite inaeleza kuwa habari zilizoandikwa jana na The Verge, The Wall Street Journal na The New York Times zinaeleza kuwa Google inataraji kuanza utoaji wa huduma ya utangazaji wa Muziki mtandaoni jambo ambalo linatarajia kutangazwa leo na kampuni hiyo wakati maofisa wake watakapokutana na watengenezaji wa programu tumishi za tarakilishi leo Mei 15,2013 mkutano ambao utafanyika Moscone Center, San Francisco utaneshwa katika sehemu mbalimbali duniani kupitia mtadaoni ambapo jijini Dar es salaam utaonekana "live" katika ofisi za KINU zilizopo barabara ya A.H.Mwinyi saa 1:00 kwa saa za Afrika Mashariki
Japokuwa Google hawajathibitisha rasmi lakini taarifa zinaonesha kuwa kampuni hiyo imeanza mchakato wa kupata leseni na Universal Music Group, Sony Music Entertainment na tayali imeshaingia mkataba na Warner Music Group ambazo zote ni Kampuni za Muziki duniani.
Times linaeleza kuwa huduma hiyo inataraji kutolewa kupitia program tumishi zinazopatikana kupitia Google Play kwa simu za Android pia kwa sasa kampuni hiyo inajipanga kutoa huduma hiyo ya muziki kupitia huduma yake maarufu ya You Tube,haya yote yanataji kufafanuliwa leo.