Saturday, May 25, 2013

PROGRAM TUMISHI 5 ZA KUKUSAIDIA KUIPATA SIMU YAKO YA ANDROID ILIYOPOTEA

Simu za Android kwa sasa zimekuwa na watumiaji wengi na inawezekana ndio zinaongoza kwa kuwavutia wezi. Lakini bila kujali kuwa simu yako imeibiwa au umeisahau sehemu kuna umuhimu wa kuhakikisha unachukua tahadhari ili inapotokea tukio linalokufanya usijue simu yako iko wapi uweze kuifatilia. Hizi ni baadhi ya software ambazo unaweza kuweka kwenye simu yako na kukusaidia pale inapopotea au kuibiwa:


1. Anti Theft Droid 
anti-theft droid

Hii ni App inayokuwezesha kufuatilia simu yako pale inapokuwa imepotea au kuibiwa. Unapoiweka katika simu yako unakuwa na uwezo wa kuifuatilia kupitia browser ya internet kama Mozilla au google chrome na inaweza kukutumia email pale inapotokea simcard ya simu yako kubadilishwa na kuwekwa nyingine. Pia inakuwezesha kuona picha ambazo zimepigwa kwenye simu yako pale unapokuwa umeipoteza.


2. Snuko – Android Anti Theft Security

snuko anti-theft

Snuko ni App inayokuwezesha kuifuatilia simu yako ya android kwa kutumia GPS, Wi-Fi na mnara wa simu inayotumia. Snuko pia inaweza kuizima simu yako pale unapogundua kuwa imeibiwa na uwezekano wa kuipata haupo na inaweza kukupa taarifa pale simcard inapobadilishwa.


3. Total Equipment Protection App
Total Equipment Protection App

Hii inafanya kazi kama nyingine zilizotajwa hapo juu ikikuwezesha kujua simu yako iko maeneo gani lakini ikiwa na kitu cha ziada ambacho ni uwezo wa kufuta data zako zote zilizokuwa kwenye simu inapotokea ukashindwa kuipata simu yako..
4. Cerberus Anti Theft
Cerberus Anti Theft

Cerberus Anti Theft inaweza kutumika kuzilinda simu hadi 5 kwa wakati mmoja, pia inakutumia taarifa kupitia ujumbe mfupi “SMS”. Kitu kingine kizuri kuhusu App hii ni kuwa inaweza kufuatilia simu yako iko maeneo gani kwa kusikiliza mazungumzo kupitia microphone ya simu yako hata kama alieichukua haitumii kupiga simu.


5. Lost Droid 

lost droid


Lost Droid ni App ambayo inakusaidia kuitafuta simu yako iliyopotea kwa kutumia computer yako. Inaweza kukutumia taarifa ya mahali simu yako ilipo kupitia SMS bila kusahau kuizima simu yako kwa kutumia SMS.
  Chanzo:tanganyikanblog

Popular Posts

Labels