Android
Mwaka huu Google imeanza kutangaza kuwa na watumiaji milioni 900 kwa watumiaji wa simu za android huku program tumishi ( Apps) zaidi ya bilioni 48 zikiwa zimetumiwa. Hili ni ongezeko la zaidi ya mara mbili tofauti na mwaka jana ambao watumiaji walikuwa milioni 400 huku kwa mwaka huu pekee programa tumishi bilioni 48 zikiwa zimetumika.
Games
Google wameiboresha Play Store kwa upande wa games ili ishindane na Apple’s Game Centre. Kwa sasa unaweza kucheza games na kulinganisha namba yako na ile ya marafiki zako ambao nao pia wameshacheza kabla yako.
Google Play Music
Google Play inaonekana kulenga kushindana na spotify ambayo ndio kwa sasa inaonekana kuongoza. Hii itawawezesha watu kucheza wimbo wowote katika simu zao au computer kwa kulipia $9.999 kwa mwezi ambayo ni kama Shilingi 16,000 za kitanzania kwa mwezi.
Google+
Google Plus ambayo ilianza kwa kishindo lakini kujikuta ikishindwa kukabiliana na ushindani wa Facebook nayo imefanyiwa mabadiliko makubwa.
Imebadilishwa kutoka kwenye muonekano wake wa tovuti na kuifanya ionekane kama program tumishi nzuri ambayo kila mtu anapenda kuitumia.
Hii inafanywa kukabiliana na Facebook ambao baada ya kuinunua Instagram wameongeza idadi ya watu waliokuwa wameanza kuikimbia kutokana na kuonekana haina jipya, Google+ inaonekana kujaribu kuongezea pale ambapo Facebook wameishia mfano katika picha wameongeza kitu kinachoitwa “Auto-Enhance” inayofanana sana na instagram filters.
Hii inaonekana kufunika zaidi kwa sababu tofauti na kubadili rangi pia inafanya mazingira yaliyokuzunguka (Background) kuonekana kwa uzuri zaidi. Google+ imewekewa kitu kinaitwa “Auto Awesome” ambayo kazi yake ni kugundua picha ambazo umezipiga kwa wakati mmoja na kwa pozi tofauti na kukutengenezea GIF ambayo safi kulinganisha na “PicMix”.
Upande wa Google Hangout ambayo ilikuwa inapatikana kwa wanaotumia computer, sasa inahamia kwenye simu zinazotumia android na iOS na pia itaongezwa extension yake katika google chrome. Hii inamaanisha Google Talk, Google+ Messenger na Google Hangout ya zamani zinaagwa rasmi. Google+ Hangout mpya inachukua rasmi nafasi na inaingizwa kushindana na WhatsApp na Facebook Messenger.
Galaxy S4 Kuwa Nexus
Google itaanza kuuza Samsung S4 ambayo ina android. Hii itakuwa na vitu vingine ambavyo mtu mwenye S4 ya kawaida anavipata lakini itakuwa na kila kitu ambacho mtu anayetumia Nexus amezoea kukiona. Hii itaingia sokoni June 26 na itakuwa na ukubwa wa 16GB.
“OK Google”
Kwa waliokwishaitumia iPhone nadhani wanaifahamu Siri, app ambayo inakupa maelekezo kwa sauti. Google nao wamekuja na kitu kinaitwa “OK Google’ ambayo itakuwezesha kupata taarifa na kukukumbusha vitu kama taarifa za usafiri, miadi na hata vitu kama vipindi vyako cha TV. Pia una uwezo wa kuifungua “OK Google” na kuiuliza chochote katika computer na yenyewe itakutafutia kila kitu hata kama ilikuwa ni kwenye Google Search.
Google Play For Education
Google imetangaza mpango wa kuhakikisha inatengeneza computer na tablet za bei rahisi kwa kila shule. Ili kufanikisha hilo imekuja na mpango inaouita Google Play For Education ambayo ni store ya program tumishi kwa ajili ya kufundishia mashuleni.
Kinachotakiwa ni kila mwanafunzi kuwa na account ya google na mwalimu atachagua program tumishi ipi gani inafaa kufundishia na kuiweka katika kila computer au tablet.
Asante kwa KINU waliofanya Live Streaming ya tukio zima na kukaribisha developers na wadau wengine wa Technology kuangalia moja kwa moja.
chanzo:tanganyikaniblog