Mwanafunzi
mwenye umri wa miaka 25 ambaye alidukua komputa za Chuo Kikuu cha Birmingham na kuongeza alama za mtihani
amefungwa jela miaka 4.
Imran Uddin, ambaye alikuwa anasoma
mwaka wa mwisho fani ya sayansi katika chuo hicho aliongeza alama za
mtihani toka asilimia 57 hadi 73 kwa kuiba neno la siri la mfanyakazi kwa
kutumia keybord inayodukua yenye uwezo kudukua komputa aliyoinunua baada ya kuitafuta kupitia mtandao wa ebay.
Kwa mujibu wa mahakama inaelezwa
kuwa Uddin alipachika nyuma ya komputa kifaa kinachoweza kuingia kwenye program ya komputa bila
mhusika kutambua.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 7 mwaka
jana ambapo kifaa hicho kilikuwa kikichukua taarifa ya kila kilichofanywa na
mtumiaji wa komputa hiyo na
baadaye ilionekana vifaa kama hivyo vilikuwa vimewekwa katika komputa
tofautikati chuoni hapo.