Friday, May 1, 2015

MFUMO WA UNUNUZI WA UMEME KUPITIA SIMU ZA MIKONONI WAVUNJWA

Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es salaam wakiwa wamepanga foleni ili kununua umeme jana

Huduma ya manunuzi ya umeme kwa njia ya miamala ya simu za mkononi nchini Tanzania imeanza kuwa kero kuanzia jana Aprili 30 mwaka huu baada ya kile kinachoelezwa kuwa ni kuvunjika kwa mkataba kati ya Shirika la Umeme Tanzania-Tanesco na mmoja wa watoa huduma hiyo ya ununuzi wa umeme yaani kampuni ya Selcom ambapo mteja hupatiwa namba ambazo huziingiza kwenye mita ya luku.

Katika mfumo huo mteja hununua umeme kupitia simu ya mkononi kupitia Mpesa, Tigo Pesa na Airtel jambo ambalo kuanzia jana haliwezekani kwa sasa ambapo kampuni ya Tigo ilianza kuwatumia ujumbe wateja wake kuwa imesitisha huduma hiyo kutokana na matatizo na wakala.

Hali ilivyokuwa:
  • Manunuzi yote ya luku yalikuwa yakifanyika kupitia mitambo ya makampuni mawili, Maxcom na Selcom.
  • Makampuni haya ndiyo yanayowapa wengine kama vile mitandao ya simu na mabenki uwezo wa kununua na kulipia huduma ya umeme -Luku
  • Hivyo mara nyingi pale ulipokuwa unapata shida kununua umeme inakuwa pale ambapo mfumo wa malipo unaotegemea mitambo ya moja ya hizi kampuni mbili unakuwa na hitilafu.
Tanesco kupitia amri ya WAZIRI wa Nishati na Madini, George Simbachawene,  na ushauri wa TRA wamevunja mkataba wa uwakala na Kampuni ya Selcom. Sababu kubwa zilizotolewa ni kutokana na mitambo yake ya kuuza umeme kwa njia hii kuwa na matatizo ikiwemo matatizo ya kisheria katika kulipa kodi.

Inasemekana kero nyingi za ukosekaji wa huduma ya manunuzi ya umeme wa LUKU ambayo imekuwa ikitokea hivi karibuni imekuwa ni kutokana na mitambo ya kampuni hii kusumbua.

Kwa kuwa kabla ya hili kutokea makampuni ya simu na baadhi ya mabenki yalikuwa yanatoa huduma hiyo ya ununuaji wa umeme kupitia mitambo ya Selcom kwa sasa utaendelea kukosa huduma hiyo.

Kwa sasa wanunuzi wa umeme kwa njia ya luku wataendelea kupata huduma hiyo kupitia vituo vya mauzo ya Luku vya Tanesco au sehemu inayouza umeme kupitia huduma ya MaxMalipo.

 credit:www.teknokona.com





Popular Posts

Labels