Gideon Msambwa akihutubia kanisani Kirumba,Mwanza |
Waumini wakimsikiliza Gideon Msambwa |
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Unioni Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Gideon Msambwa ametoa ushauri kwa washiriki kutumia teknolojia ya habari na mawasilino ili kuleta maendeleo ya kanisa hilo nchini.
Akizungumza jana Mei 9 mwaka huu jijini Mwanza katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Kirumba,Msambwa amesema Mataifa ya Asia na Kusini mwa Bara la Amerika yamepiga hatua kubwa katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,hadi kufikia hatua ya kumiliki viwanda.
Akitoa mfano, amesema Kanisa la Waadventista wa Sabato Korea Kusini linamiliki viwanda vidogo 104,000 wakati Tanzania bado kanisa hili linamiliki kiwanda kimoja cha Uchapaji kilichopo mjini Morogoro.
Amesema pia kwamba, Korea Kusini kuna vyuo vikuu vitano vya Kimataifa,wakati hapa nchini Waadventista wa Sabato wanamiliki Chuo kikuu kimoja,University of Arusha.
Korea Kusini kanisa hili humikili kiwanda bora cha uchapaji,wakati nchini Brazil kanisa hili washiriki wake wamepiga hatua kubwa katika medani ya elimu na teknolojia.
Mkuu huyu wa Mawasiliano katika Union Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania,amesema asilimia 60 ya wabunge Brazil ni Waadventista wa Sabato,huku washiriki wa kanisa wameunganishwa katika Mfumo wa kiteknolojia wa kutunza kumbukumbu uitwao,Adventist Church Manegement System(ACMS),ambamo kumbukumbu zote za washiriki na wachungaji hutunzwa.
Kufuatia hali hiyo,Tanzania na Ghana zimechaguliwa na Konferensi Kuu(GC) kuandaa mfumo huu wa kutunza kumbukumbu.
Hadi sasa, Union 38 hapa duniani za kanisa hilo kumbukumbu zake zimehifadhiwa katika Mfumo huu wa ACMS.Jumla ya washiriki waliobatizwa wa Kanisa 7,500,313 kumbukumbu zao zinahifadhiwa katika mfumo huu duniani,miongoni mwa hawa 1,679 ni wa makanisa 1,735 ya Unioni ya Kaskazini mwa Tanzania.
Unioni ya Kaskazini mwa Tanzania(NTUC) ina jumla ya washiriki waliobatizwa 354,456 wakati washiriki wengi kumbukumbu zao zikiwa hazijaingizwa katika mfumo huu mahsus wa kumbukumbu.
Kufuatia hali hiyo,Idara ya Mawasiliano ya Unioni hii imewataka wachungaji na washiriki kuhakikisha kuanzia sasa hadi Disemba 2016 asilimia 50 ya kumbukumbu zote za washiriki ziwe zimeingizwa katika mfumo huu.