Mwaka 2013, Mwenyekiti Mtendaji wa Google Eric Schmidt alikisia kuwa duniani kote watu watakuwa kwenye mtandao mwishoni mwa karne.
Kuna progam tumishi nyingi ambazo zimetengezwa na zinatengezwa zikijaribu kuwaweka watu karibu kwenye mitandao .
Ripoti iliyolewa hivi karibuni inaonesha kuwa kuna baadhi ya program tumishi ambazo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kuwaweka mtandaoni mamilioni ya watu duniani miongoni mwa program hizo maalufu ambazo zinaonekana kuongoza kupitia simu za mikononi ni;
1. M-Pesa
Hii ni Program tumishi kwa ajili ya malipo kupitia simu za mkononi ambayo inatumika barani Afrika huduma iliyoanzishwa mwaka 2007 na kampuni ya Safaricom ya nchini Kenya iliyomiongoni mwa makampuni ya Vodafone,Mtumiaji anaweza tuma ama kupokea fedha kupitia ujumbe mfupi wa maneno,kulipa bili na kununua muda wa maongezi.Katika maeneo ambapo watu wanapata huduma chache za kibenki ama hakuna huduma hizo M-Pesa imekuwa ikipata umaarufu ambapo kwa sasa inaonesha kufikisha kiasi cha watumiaji milioni 18 wa huduma hiyo.
2. SoukTel
Ikiwa inatumika Mashariki ya Mbali, SoukTel ina program tumishi mbalimbali zinazowasaidia watu kupata taarifa kuhusu kazi na huduma za kijamii.Inajuikana hasa kwa kuhusianisha katika kutafuta kazi na inawaunganisha watu mbalimbali kupitia ujumbe mfupi wa maneno toka Jordan,Rwanda,Tunisia na nchi mbalimbali.Hivi karibuni SoukTel iliungana na Facebook na kuanzisha huduma ya elimu ya uchumi nchini Colombia.
3. Esoko
Mara nyingi huelezwa kuwa ni Facebook kwa ajili ya wakulima Esoko inawaunganisha wakulima na mashirika yasiyo ya kiserikali,makampuni ya biashara na wakala wa serikali .Soko ni neno la kiswahili linalotokana na sokoni na E ikisimama badala ya vifaa vya umeme.
Utumaji wa ujumbe mfupi wa maneno kwa kuhusianisha tovuti ambapo hutuma taarifa kuhusu hali ya hewa,taarifa za bei na matangazo.
4. Frogtek
Kwa kutumia program za simu za kisasa na tabiti, Frogtek inasaidia wafanya biashara wadogo hasa katika familia ndogo maarufu mom-and-pop katika nchi za bara za Amerika ya Kusini na baadhi ya nchi zinazoendelea ambapo huwawezesha wafanyabiashara hao kufahamu bidhaa walizonazo na mauzo yaliyofanyika
5. Ver Se’ Innovation
Imetengenezwa huko Bangalore, India,ni program tumishi ambayo ni maalum kwa taarifa na huduma za ndani ya India ambayo husaidia kutoa taarifa za kazi,umiliki wa vitu mbalimbali na matangazo ya masoko huku ikiwa na huduma ya malipo na manunuzi kwa njia ya mtandao.