Friday, June 5, 2015

TANZANIA KUATHIRIKA ZAIDI NA UHALIFU MTANDAO

 
Yusuph Kileo akitoa mada kwenye mkutano huo
Mazungumzo ya awali kabla ya mkutano wa wanausalama mitandao uliokamilika jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini yanaweza kusomeka kwa "KUBOFYA HAPA"  Mkutano ambao uliokua na vuta nikuvute kupata suluhu ya changamoto tulizo nazo za kiusalama mtandao duniani kote zinazoendelea kukua kila kukicha huku ikionekana dhahiri kabisa wahalifu mtandao wanaelekea kuzidi nguvu huku Tanzania ikiorodheshwa kuwa ya sita kwa nchi zinazotegemewa kuathirika zaidi na uhalifu mtandao barani Afrika.

Akitolea ufafanuzi wa takwimu hizi Bwana Vernon Frye, Mkuu wa Usalama mitandao wa kampuni ya Vodacom ya Afrika Kusini, alielezea kuhusiana na uhalifu mpya wa Ransomware ambapo tayari athari zake zimesha onekana Nchini huku akiibua mjadala mzito wa wapi tume jikwaa.
 
Aidha Mjadala mrefu kutoka kwa aliyekua Mkurugenzi wa wakala wa usalama wa Marekani (National Security Agency – NSA) Bwana William Binney pamoja na Raisi na muanzilishi wa kivinjari cha aina ya Tor kinachotumika sana na jumuia ya wana usalama mitandao waliibua changamoto ya ufaragha baina ya watumiaji wa mitandao na namna ya kuendelea kuhakiki kunapatikana uthibiti wa faragha hizi kutotumika vibaya na wahalifu.
 
 
Akiwasilisha mada ya changamoto tulizo zazo barani Afika na nini kifanyike ili kujikwamua katika hali mbaya tuliyo nayo hivi sasa ya wimbi la uhalifu mtandao barani afrika ambapo umeendelea kugharimu bara katika Nyanja za kisiasa, kijamii pamoja na kiuchumi. Yusuph Kileo toka Tanzania alielezea kwa kina mambo ya msingi tunayo takiwa kuyafanyia kazi ili kuhakiki Bara linabaki salama.

Katika mjadala huu ambapo wanausalama mtandao kutoka maeneo mbali mbali ya dunia waliunga mkono alichozungumza kuwa bado kuna kusua sua katika ushirikiano wa pamoja katika kutokomeza uhalifu mtandao huwa wahalifu mtandao kuonekana niwenye ushirikiano ulimkubwa kabisa.
 
Aidha alifafanua kuhusiana na mipango isiyo endelevu ya kukuza vipaji vya wana usalama mtandao wa ndani pamoja na kuwa na program za kukuza uelewa kwa jamii juu ya matumizi salama mitandao ambazo hazionyeshi athari kutokana na uhaba wa maandalizi sahihi na kujua walengwa stahiki.

Makubaliano yamsingi yalikua ni mengi na kwa uchache ni pamoja na kuhakiki kunakua na program endelevu za kuwa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao sanjari na kukuza wataalam wa ndani. Pia Ushirikiano baina ya wanausalama si tu katika ngazi ya kitaifa na kibara bali kidunia imeonekana ni muhimu sana. Aidha makampuni kuhakiki yanatumia teknolojia zinazoweza kuendana na hali ya uhalifu hivi sana na kuhakiki wanaziba mianya ya kihalifu kuanzia kwa wafanyakazi wao imeonekana ni jambo muhimu sana.
 
Aidha mkutano huo ulitoa fursa ya washiriki kupata kubadilishana mawazo kwa nyakati tofauti ambapo mtaalamu huyo wa masuala ya usalama katika mitandao alitumia fursa hiyo kuweza kujifunza mengi kutoka kwa mkongwe wa fani hii na aliyeweza kuongoza wakala kubwa ya usalama mitandao ya nchi ya Marekani kama inavyo onekana pichani.
 
 
 

Popular Posts

Labels