Laini za simu za mitandao ya simu nchini Tanzania ambazo hazijasajiliwa zitazimwa rasmi Julai 10, mwaka huu.
Naibu Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema hayo Bungeni
jana, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na matumizi mabaya ya simu.
Alisema serikali pia imekamilisha kanuni na Sheria ya Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta (Epoca) zitakazodhibiti matumizi mabaya ya simu za
mkononi.
“Serikali pia inashirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwasaka na kuwakamata
wote wanaotumia simu vibaya,” alisema.
Makamba alisema Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ilifanya usajili wa namba za watumiaji wa simu za mkononi ambapo hadi sasa namba za simu 24,399,000 zimesajiliwa.
“Usajili wa namba za simu pamoja na masuala mengine, ulikuwa na lengo la
kupunguza matumizi mabaya ya simu za mkononi,” alisema.
Makamba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM), ambaye alitaka kujua serikali inasema nini juu ya baadhi ya watu kutumia simu za mkononi kusambaza ujumbe mfupi na maneno ya kuzusha.
chanzo:mwanamakonda blog